Thursday, April 16, 2015

Baada ya hapo jana kutangaza kuwa ataachana na klabu ya  Borussia Dortmund mwishoni mwa msimu huu,kocha Jurgen Klopp amefunguka tena na kusema hatachukua muda wa mapumziko kama wengine wanavyodhania.
Kocha huyo alitua klabuni hapo mwaka 2008,ameiwezesha klabu hiyo kuchukua ubingwa wa Bundesliga mara 2,mwaka 2011 na 2012 na ubingwa wa DFB Pokal na pia kuiwezesha timu hiyo kushika nafasi ya pili katika michuano ya klabu bingwa Ulaya msimu wa 2012/2013.
Klopp,47, amesisitiza kuwa hatafanya kama Pep Guardiola ambaye alipumzika kwa mwaka mmoja baada ya kutoka katika klabu ya Barcelona mwaka 2012.
Taarifa hiyo imewastua watu wengi na kuwafanya wadau wa soka kudhani kuwa kocha huyo atachukua mikoba ya Manuel Pellegrin ambaye anasuasua katika klabu ya Manchester City. "Siyo kwamba nimechoka, pia sijafanya mazungumzo na klabu yoyote mpaka sasa. Sihitaji kuchukua mwaka mmoja wa mapumziko" alisema Klopp.
Baada ya kutolewa katika michuano ya klabu bingwa msimu huu,klabu ya Borussia Dortmund inayoshika nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi kuu nchini Ujerumani sasa inajitahidi kufanya vizuri ili waweze kumaliza wakiwa katika nafasi za juu kunako ligi hiyo.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video