Saturday, April 11, 2015



Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
JUZI na jana tuliangalia sababu tatu zilizoiponza Coastal Union FC na kujikuta ikishushiwa kipigo kikubwa cha mabao 8-0 dhidi ya Yanga SC Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumatano.

Kwa kujikumbusha, tuliangalia kuhusu kikosi kilichocheza ambacho hakikuwa na wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza cha Wagosi wa Kaya, tukatazama kuhusu makundi na mabadiliko ya mara kwa mara ya benchi la ufundi.

Leo tunamalizia suala hili kwa kuangalia sababu nyingine mbili zilizopelekea kutokea kwa aibu hiyo kwa mabingwa wa 1988 wa Tanzania Bara.

Nne, kutokuaminiana kuliigharimu Coastal dhidi ya Yanga SC Jumatano. Ikumbukwe kuwa muda mfupi kabla ya mechi dhidi ya Azam FC Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga Machi 22 mwaka huu, baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Coastal waliondolewa kikosini.

Aliyekuwa kocha mkuu, Mkenya James Nandwa na msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo 'Julio' walipanga kikosi ambacho hakikuwa na nyota sita wa kikosi cha kwanza kuivaa Azam FC.

Kipa mzoefu Shaaban Kado hakupangwa pamoja na nyota wengine watano wa 'First 11'. Kipa Bakari Fikirini alikaa langoni na kufungwa bao rahisi dhidi ya mshambuliaji John Bocco 'Adebayor'.

Taarifa ambazo mtandao huu ulizinyaka kutoka kwa baadhi ya viongozi wa Coastal, zilidai kuwa Kado na baadhi ya nyota wengine wa kikosi cha kwanza cha Coastal, hawakupangwa kucheza mechi dhidi ya Azam kwa madai kuwa walikuwa wamepanga kuihujumu timu yao.

Kado baada ya tuhuma hizo aliondoa Tanga na kurejea kwake, Bonyokwa jijini Dar es Salaam kabla ya kurejea siku chache kabla ya kuivaa Yanga SC, lakini hakuwamo hata kwenye orodha ya wachezaji wa akiba wa Coastal kwa ajili ya kuivaa timu hiyo ya Jangwani Jumatano.

Je, umejiuliza kwa nini Lutimba Yayo na Itubu Imbem hawakuwapo katika kikosi cha Coastal kilichoivaa Yanga SC Jumatano? Kwa nini wachezaji hao wa kutegemewa katika kikosi cha kwanza, hawakuwapo hata benchini siku hiyo? 

Taarifa zilizoufikia mtandao huu zimedai kuwa nyota hao wamelazimika kujitoa kikosini kutokana na tuhuma zinazoelekezwa kwao na baadhi ya watu ndani ya klabu hiyo ya Pwani, kwamba wanaihujumu timu.

Kwa kifupi, kumetokea kukosekana kuaminiana miongoni mwa wachezaji, makocha na viongozi wa Coastal Union FC ndiyo maana hata kikosi kilichopangwa Jumatano na Julio kilikuwa na wachezaji wengi ambao si wa kikosi cha kwanza.

Tano, ubora wa kikosi cha Yanga SC. Coastal Union FC ilikutana na Yanga SC ambayp ilikuwa imekamilika karibu kila idara.

Ikumbukwe kuwa, ukimwondoa beki wa kati Kelvin Yondani, wachezaji wengine wote walioanza Jumatano ndiyo walioanza katika mechi ya Jumamosi nchini Zimbabwe dhidi ya FC Platinum.

Kikosi hicho kilifungwa bao 1-0 ugenini na kipindi cha pili FC Platinum walilazimika kucheza kwa kupaki basi, hususan baada ya kuingia kwa winga Mrisho Ngassa.

Yanga imepoteza mechi moja tu Uwanja wa Taifa, tena dhidi ya watani wao wa jadi, Simba SC na iliifunga Coastal bao 1-0 jijini Tanga katika mechi ya kwanza ya Ligi ya Bara Februari 4, mwaka huu.

Coastal Union FC wamekutana na Yanga SC ambayo ilikuwa imefunga mabao mengi zaidi (28) na kufungwa machache zaidi (11) kuliko timu nyingine katika Ligi ya Bara.

Kikosi cha Julio kilikutana na Yanga SC ambayo ina mfungaji bora wa ligi msimu uliopita na mfungaji bora wa Kombe la Kagame 2013, Amissi Tambwe.

Yanga SC pia ilikuwa na kinara wa mabao, Simon Msuva na mchezaji bora wa ligi misimu miwili iliyopita, Yondani.

Kwa kifupi, Coastal walikutana timu ambayo inaoongoza kwa kila kitu kizuri katika ligi kuu msimu huu huku ikijiandaa kwa mechi ngumu ya kimataifa dhidi ya Etoile Sportive du Sahel (ESS) ya Tunisia.

Sita, kauli la za Julio kabla ya mchezo zilioneshwa wazi Coastal ilikuwa ingeshindiliwa mabao mengi na Yanga SC.

Siku moja kabla ya mechi, Julio alisema kikosi chake hakikujiandaa kwa ajili ya mechi hiyo kwa madai kuwa ratiba waliyokuwa nayo ilionesha mechi ingechezwa Aprili 18 mwaka huu.

Kibaya zaidi, Julio akaweka wazi kwamba hategemei kushinda mechi hiyo na kwamba Yanga SC walikuwa wanakwenda kupata ushindi.

"Nilikuwa kwenye bonanza la Pasaka Jumatatu, napigiwa simu na uongozi kwamva niandae timu kwa ajili ya kucheza na Yanga Jumatano. Hadi nilifikia hatua ya kugombana na viongozi," alisema Julio.

Katika hali kama hiyo, ni wazi kwamba Julio aliwaandaa wachezaji wake kwenda kushiriki mechi na si kushinda na haikushangaza kuona matokero ya 8-0 dhidi ya Yanga SC.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video