Friday, April 17, 2015

Okwi atawakosa Mbeya City fc kesho

MBEYA CITY FC kesho inaikaribisha Simba katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara itayopigwa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Afisa habari wa Simba, Hajji Sunday Manara amesema kesho ni kufa na kupona ili kuvuna pointi tatu muhimu mbele ya timu iliyojeruhiwa na Yanga.

"Pointi tatu kwetu muhimu sana, tunaanza na kesho, kisha tunasubiri 12 zilizosalia. Unajua kando ya matakwa ya Mungu hizo pointi 15 hazizuiliki, hakuna chochote cha kutuzuia hizi sasa" Amesema Hajji na kuongeza: "Unajua kwa mfumo wa Simba inategemea zaidi kushirikiana kwa pamoja 'team-work', hatutegemei vipaji vya mtu mmoja mmoja".
Simba itamkosa mshambuliaji wake muhimu, Emmanuel Okwi mweye kadi tatu za njano, lakini Simba haina wasiwasi juu ya hilo ingawa wamekiri kuwa ni mchezaji muhimu.
"Ni kweli Emmanuel Okwi ni pengo kubwa kwasababu yeye ni mchezaji mkubwa, ni  kiwango kingine, anajitofautisha na wachezaji wengi waliopo katika timu zote za ligi,  kwa mfumo wa mwalimu, bila shaka pengo lake litazibwa tu. Tuna wachezaji wengi ambao wako vizuri, unakumbuka mechi ya mwisho na Kagera Sugar tulikosa wachezaji saba wa kikosi cha kwanza na tulishinda goli 2-1 ugenini, kwahiyo hilo halitupi tabu"

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video