Na mwandishi wetu
Ukifumba macho na kuangalia miezi takribani
sita au saba iliyopita unaweza leo hii ukabaki mdomo wazi,
kipindi hicho Mtibwa sugar ilikuwa
inaongoza ligi ya Tanzania na ndicho kipindi Mecky Mexime alikuwa anaonekana
kocha bora mpaka wenye matege yakufikiri wakawa wanapendekeza apewe timu ya
taifa na
mwenyewe Mexime ndicho kipindi alichokuwa anaropoka hovyo na hata
kufikia hatua kuwaponda makocha wenzake, lakini wachache tulibaki tu
kumsikiliza na kujiuliza kwa ukocha gani alionao? lakini hivi tunavyozungumza Mtibwa
inapigania kushuka daraja na Mexime mdomo ameufyata lakini pia ukifumba macho
na kuiangalia ligi ya msimu uliyopita, utaona jinsi Mbeya city walivyoleta
amsha amsha
katika ligi ya tanzania na style yao yakurudisha wanachokipata kwa
wananchi wahitaji, mashabiki wao walikuwa na style yakwenda
mahospitalini kuwaona na kuwafariji wagonjwa na mwisho wa siku waliweza kujitolea
kufanya usafi katika jiji lao, watu tukasema sasa timu ya kijamii imepatikana...
Lakini kilichotea hivi sasa kila mtu
anashika kichwa, walianza kutimuana wenyewe kwa wenyewe, siasa za kimkoa
zikawatafuna hatimaye
wamepotea na usishangae msimu ujao tukawakuta wakiwa katika nafasi yakupigania
kutoshuka daraja..
Haya siyo mapya kwa sisi tuliokula chumvi
nyingi kidogo kuyaona katika ligi ya tanzania, kulikuwepo na timu nyingi tu za aina
hii, kwa kawaida timu kama hizi, tunaziita "timu mlipuko" walikuwepo
kajumulo fc, chini ya tajiri wa kitanzania Alex Kajumulo ambaye maisha yake
yalikuwa pale Marekani na ambaye alikuwa mwanachama wa Simba alikuja kwa
mbwembwe kubwa, Tukuyu Stars, Parsons chini ya tajiri ambaye alikuwa anamiliki
migodi ya dhahabu na alikuwa mwanachama wa Simba, ushirika Moshi, hawa wote walikuwepo
na wamepotea... tatizo ni nini?
Tatizo kubwa linaloziathiri timu hizi
mlipuko ni moja tu...nalo ni malengo
yao yakuwepo ligi kuu malengo yao siku zote hayawi katika kuchukua kombe la
ligi kuu bali malengo yao ni kuja kushindana na Yanga na
Simba, hasa hasa Yanga, hapo ndipo wanapoanza wenyewe kujipoteza...
ukiiangalia Azam fc utaona kama ni klabu ambayo ipo kisasa zaidi ni kweli
ina kila kitu tena kuzishinda klabu nyingi na muda mwingine hata ulaya
kwenyewe, lakini zaidi yakuchukua kombe
la ligi kuu ya vodacom nini
kingine hasa ambacho wanaweza kusimama mbele ya watu na kujivunia na utajiri
wote ambao wanao?
Malengo ya uanzishwaji wa azam yalikuwa yapi?
kwanza ieleweke Azam ni chimbuko la
timu ya wafanyakazi wa Bakhresa Group of Campanies ambao waliamua kuunda timu yao
kwa ajiri ya kujifariji baada ya kazi ngumu za kukanda unga wa chapati na kuuza
juice, mwisho wa siku waliamua kununua haki za kipawa Combine fc, na rasmi kuanza
kushiriki ligi za ngazi ya chini mzee Bakhresa ambaye ni mshabiki na mwanachama
mkubwa wa Simba alipoona mawazo yake yakuiendesha klabu ya simba kisasa
yamekataliwa ndani ya Simba ndipo rasimi alipoamua kuwekeza nguvu kwa azam
akiwa na lengo kuu
lifuatalo; kuhakikisha azam na simba wanashika nafasi mbili za juu huku Yanga
ikishika kuanzia nafasi ya tatu, ndipo alipokuja na sera zakubadilishana na
kuuziana wachezaji wa simba kwenda azam na wa
Azam kwenda Simba...
Hii ndiyo sumu kubwa ambayo Azam walijitengenezea wenyewe na kuamua kuinywa,
ingawa Yanga ilipitia misukosuko mingi ikiwemo Azam kuingiza mkono katika mechi
nyini za Yanga lakini haikusaidia kitu zaidi yakuiacha yanga ikiwa imara zaidi
na kuendelea kubaki katika nafasi mbili za juu, huku swahiba mkuu Simba akibaki
kupotea katika mbili
bora...
Maji sasa yamezidi unga kwa Simba wamechoka sasa nao wanaitaji
kujikwamua kutoka katika aibu ya kila mwaka ya kukosa nafasi mbili bora ndipo tunapoona
ndugu kwa ndugu wameanza kuombeana mabaya, Simba sasa anamuombea Azam apoteze
mechi zake ili apate nafasi ya pili na azam naye anamuombea simba apoteze mechi
zake ili apate nafasi ya pili wote hawa hakuna anayemuombea yanga apoteze mechi
zake kwa sababu wanajua wazi Yanga haiwezekani tena...
Azam kabla yakupambana na Yanga alipaswa kwanza kujua asili na chanzo
cha mkubwa wake simba, Simba ni zao la yanga ata jina lenyewe la Simba lilipendekezwa
na mwanachama namba moja wa Yanga mzee Karume rais
wa kwanza wa Zanzibar siku zote ninawaheshimu Yanga, Azam
wasipobadilika kimtazamo nao watapotea na uwanja wa Chamanzi
utabaki kama sehemu ya kuhifadhia makontena au maonyesho kuwa
kulikuwepo na timu ya Azam dalili zinaanza kuonekana, hatua ya juzi,
siku walipocheza na Mbeya city viongozi wao kutukanana hadi kushikana mashati ni
dalili tosha....
Siku zote chenye nguvu kina maisha marefu
na kinadumu
0688665508

0 comments:
Post a Comment