Rodriguez akishangilia goli lake
Timu ya Real Madrid imezidi kuipumulia kwa ukaribu na kuongeza presha kwa viongozi wa ligi kuu ya Hispania timu ya Barcelona baada ya kushinda goli 3-0 dhidi ya Almeria. Magoli ya Madrid yamefungwa na James Rodriguez dakika ya 45 likafuatiwa na goli la kujifunga la mchezaji wa Almeria Santos dakika ya 49 kabla ya Arbeloa kuhitimisha idadi hiyo ya magoli dakika ya 84.

Tumeshuhudia mbinu na matukio mengi sana yakitokea katika mpira wa miguu lakini hili lililotokea katika mechi kati ya Real Madrid dhidi ya Almeria ni baba lao.

Usiku huu katika mechi iliyowakutanisha vijana wa Carlo Ancelott Real Madrid na Almeria hasa pale mpira ulipotoka na kutakiwa kurushwa ndipo mlinzi kwa kushoto Fabio Contreao na James Rodriguez wote walipochukua mipira na kuirusha pamoja uwanjani kwa wakati mmoja tena kwa ustadi mkubwa,
Hii ni mara ya kwanza Dunia kushuhudia mipira miwili ikirushwa kwa pamoja uwanjani wakati mchezo ukiendelea.
MATOKEO YA MECHI NYINGINE ZILIZOMALIZIKA
FT
FT
0 comments:
Post a Comment