Monday, March 2, 2015


 Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Uongozi wa Yanga SC umesema hauna hofu yoyote kuelekea mechi yao ijayo watani wa jadi kwani Simba SC kwa sasa si mpinzani wao.

Aidha, uongozi wa wanajangwani umesema kambi ya kikosi chake iliyowekwa Bagamoyo, Pwani si kwa ajili ya kujiandaa kwa mechi ya Jumapili dhidi ya Simba SC, bali ni maandalizi ya mechi ya Machi 14, mwaka huu dhidi ya Platinum ya Zimbabwe kwenye Uwanja wa Taifa jijini hapa.

Yanga SC iliyopoteza mechi iliyopita dhidi ya BDF XI FC nchini Botswana, itakuwa na kibarua kigumu mbele ya Simba SC inayopigana kurejesha heshima yake katika Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL), watakapokutana Uwanja wa Taifa jijini hapa Jumapili.

Jerry Muro, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, ameuambia mtandao huu jijini hapa muda mfupi uliopita kuwa hawana hofu yoyote kuelekea mechi hiyo kwa kuwa Simba SC si wapinzani wao kwa sasa.

"Mpinzani wetu kwa sasa ni Azam FC, Simba watabaki kuwa watani wetu, lakini si wapinzani wetu maana hawana nafasi ya kutufikia kileleni mwa msimamo wa VPL," Muro ametamba.

"Hata kama wangeweka kambi nje ya mipaka ya Tanzania, bado wasingeweza kututisha ndiyo maana tunawasubiri hapa hapa Dar es Salaam.

"Timu iliingia kambini Gagamoyo jana mara tu baada ya kurejea kutoka Botswana. Simba wala hawatuumizi vichwa kwa sasa.

"Kambi yetu inayoendelea kwa sasa mjini Bagamoyo si kwa ajili ya mechi dhidi ya Simba, bali maandalizi ya mechi ya kimataifa dhidi ya Platinum ya Zimbabwe," amesema zaidi Muro.

Kikosi cha Simba SC kinachonolewa na Mserbia Goran Kopunovic, kiliingia kambini visiwani Zanzibar juzi kunoa makali kabla ya kumenyana na Yanga SC ambao katika miaka ya karibuni wamekuwa wakisotea ushindi dhidi ya kikosi hicho cha Msimbazi.

Simba SC ilishinda mabao 5-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mechi yake iliyopita Uwanja wa Taifa, kikiwa ni kipigo kikubwa zaidi msimu huu wa ligi kuu ya Bara

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video