Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Saa chache baada ya kutangaza kumtimua kocha mkuu Joseph Omog na mmoja wa wasaidizi wake, Ibrahim Shikanda, uongozi wa Azam FC umeeleza SABABU za kuachana na wataalam hao wa ufundi.
Muda mfupi baada ya timu kuwasili jijini hapa ikitokea Khartoum, Sudan ambako imeng'olewa dhidi ya El Merreikh katika michuano ya kimataifa, uongozi wa Azam FC umetangaza kuwafukuza kazi Omog na Shikanda.
Jaffar Idd Maganga, msemaji wa Azam FC, ameuambia mtandao huu kuwa, wamefikia uamuzi huo baada ya kukiukwa kwa matakwa ya kimkataba kati ya klabu na makocha hao.
"Taarifa ambazo nimepewa na uongozi ni kwamba, Omog na Shikanda wameondolewa kwenye benchi la ufundi la Azam FC na kocha George Nsimbe ndiye aliyekabidhiwa timu," Maganga amesema na kuongeza:
"Sababu kubwa ya kuachwa kwa makocha hao ni kukiukwa kwa masharti ya mkataba kati yao na klabu. Katika mkataba wa Omog, kuna kipengele kinatamka wazi kwamba ataipa mafanikio timu katika michuano ya kimataifa. Na mkataba wa msaidizi wake (Shikanda) ulikuwa na kipengele hicho pia.
"Kufanya vibaya kwa timu yetu katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika 'automatically' (moja kwa moja) ni kukiukwa kwa masharti ya kimkataba kati yao na klabu," amesema zaidi Jaffar.
Azam FC, licha ya kushinda 2-0 nyumbani wiki mbili zilizopita, wameondoshwa katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya El Merreikh ugenini Uwanja wa Khartoum, Sudan Jumamosi usiku.
Kabla ya mechi hiyo dhidi ya El-Merreikh, Azam ilitoka suluhu mara mbili dhidi ya Ruvu Shooting Stars na Tanzania Prisons Stars, huku kiwango cha timu kikionekana kushuka kwa kiasi kikubwa tangu kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara Septemba 20, mwaka jana.
Azam FC iliingia mkataba na Omog ikiwa na matumaini ya kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa, lakini kibao kimegeuka na kuambulia ushindi mmoja wa nyumbani, huku timu ikicheza kwa kiwango cha chini katika michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar miezi miwili iliyopita.
Omog amekuwa kocha mkuu wa tatu kuondoka Azam FC ndani ya misimu miwili tangu kutimuliwa kwa Boris Bunjak na kuondoka kwa Muingereza Stewart Hall msimu uliopita.
Makocha wakuu wengine waliotimuliwa na timu za Ligi Kuu Bara msimu huu ni Dennis Kitambi wa Ndanda FC na Patrick Phiri wa Simba SC, huku aliyekuwa kocha mkuu wa Stand United FC, Emmanuel Masawe (kaka wa mchezaji bora wa ligi hiyo msimu wa 2011/12 Jacob Masawe akiwa na Toto Africans ya Mwanza - sasa anakipiga Ndanda FC) akisimamishwa.

0 comments:
Post a Comment