"Wao wanajifanya wana hela, sisi tunapambana nao tunavyojua sisi. Huwezi kuwatenga wazee wa klabu kama Hamis Kilomoni, halafu unamuweka Hassan Dalali kwenye kundi la wadhamini. Kilomoni ameichezea Simba, anaijua Simba tangu inaitwa Sunderland, kawa katibu mkuu na kufanya kazi iliyotukuka, leo unaanzaje kumwambia sio Simba?"
"Tulipoenda Shinyanga tulisema tunapigwa, tukapigwa, tukaseme twendeni Dar na tukawaambia tunapiga mtu 5-0, wakasema aaah wapi! jana tukapiga 5-0."
"Wanaendelea na mkutano leo, sijui watajadili nini na kuamua nini juu yetu. Tulishapokonywa kadi, watakachoamua sawa, lakini lazima wajue kwamba tutapambana nao kama wataendelea kutukorofisha, sisi ni wapole sana"
"Wanawatuma watu watufanyie vuruguru, sisi tunawajua wote. Wakiendelea kuleta jeuri tunashusha timu daraja. Sio sisi tunaofanya kazi hiyo, ni wazee, sisi tumebeba tu matatizo. Wakae chini nao na kuwarudisha klabuni".
Haya ni maneno ya kigogo mmoja wa kundi la Simba Ukawa akiongea na mtandao huu wakati wanachama na viongozi wa Simba wamekutana katika mkutano mkuu unaofanyika muda huu Ukumbi wa Bwalo la Polisi Osterbay, Dar es salaam kujadili mwenendo wa klabu hiyo katika michuano ya ligi kuu.
0 comments:
Post a Comment