Sunday, March 1, 2015

WATU wa El Merreikh mjini Khartoum, Sudan wamewaambia Azam FC, hata waende kulalamika wapi, Shirikisho la Soka
Afrika haliwezi kuwasikiliza kwa kuwa kuna mtu anaitwa Magdi Shams El Din (pichani juu).
Azam FC jana imeaga mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kufungwa mabao 3-0 na El Merreikh ya Sudan katika mchezo wa marudiano wa Raundi ya Awali
uliofanyika Uwanja wa Marreikh mjini Khartoum.

Marefa wa mchezo huo kutoka Zambia Wellington Kaoma aliyesaidiwa na Romeo Kasengele na Amos Nanga walionekana wazi kuiuma Azam FC katika mchezo huo.
Pamoja na kupewa penalti ambayo ilipigwa na Augustine Okran na kuokolewa na kipa Aishi Manula, Merreikh ilimaliza dakika 45 za kwanza inaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa ba Bakr dakika ya 16.
Kipindi cha pili marefa wa Zambia waliongeza mbeleko kwa Merreikh na ikafanikiwa kupata mabao mawili zaidi yaliyofungwa na Ahmed Abdallah dakika ya 85 na Alan Wanga dakika ya 90.
Azam FC inatolewa kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya awali kushinda 2-0 katika mchezo wa kwanza nyumbani, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Kwa kujua mbinu walizopanga na marefa hao, Merreikh walizuia mchezo huo usionyeshwe na Televisheni yoyote.
Na baada ya mchezo huo, Azam FC walianza jitihada za kuwasilisha malalamiko yao kwa Kamisaa, Ahmed Mohamed
Magahed Osman wa Misri lakini hawakusikilizwa.

Kamisaa huyo alikuwa akiongea kwa kicheko na furaha na viongozi wa Merreikh na watu wa timu hiyo ya Sudan wakawaambia kwa Kiingereza viongozi wa
Azam FC; “Mtakwenda popote hamtafanikiwa, kuna Magdi Shams El Din,”.

Magdi Shams El Din ni Msudan, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Marefa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ambayo
inahusika kupanga marefa kwenye mashindano.

Hakuna refa ambaye anaweza kupuuza agizo la Magdi Shams El Din kwa sababu anajua ataishia kuchezesha Ligi za nchini
mwao na kwa sababu hiyo kuna uwezekano marefa wa Zambia waliweka pembeni sheria 17 za soka katika mchezo wa jana ili ‘kumfurahisha’ bosi wao, Magdi Shams El
Din.

Lakini pamoja na ‘mikwara’ hiyo, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba mwenye uzoefu wa kuanzia kufanya kazi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amesema wanapelekea kesi na ushahidi wote CAF juu ya udhalimu waliofanyiwa na Merreikh na marefa wa Zambia.
Kwa ujumla, matendo yote waliyofanyiwa Azam FC nchini Sudan toka siku ya kwanza walipowasili nchini humo hayakuwa ya kisoka na yamefananishwa na matendo ya
kigaidi ndani ya mchezo wa soka.

Ikumbukwe pia siku walipofika walipokewa na longolongo nyingi uwanja wa ndege na walisumbuliwa sana ikiwa ni pamoja na kucheleweshewa visa zao, lakini pia hata gari walilopokelewa lilikuwa ni bovu sana kama vilie la kubebea mkaa.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video