Sunday, March 1, 2015

MASHABIKI zaidi ya 2000 wa City waliokuwa wamejazana kwenye uwanja wa Sokoine kushuhudia mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting ya Mlandizi Pwani, wamesifu kiwango cha mlinda mlango Hanington Kyalesebula  aliyekuwa  langoni kuitumikia  timu yake kwa mara ya kwanza.
Kwa muda mrefu, Kipa David Buruhani alikuwa chaguo la kwanza la kocha Juma Mwambusi, lakini kufungwa mabao 3 katika mechi dhidi ya Yanga uwanja wa Sokoine, februari 22 kulimfanya aondolewe kikosini na sasa kama ameanza kushaulika.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo mashabiki hao walisema kuwa walikuwa hawana uhakika wa golikipa yupi kati ya wanane waliopoa atasisimama imara kulinda milingoti mitatu ya lango la City hasa  baada ya kupumzishwa kwa David Buruhani aliyekuwa chaguo la kwanza hapo kabla.
“Kwa kweli amecheza vizuri,  tunamshukuru kwa hilo, pengine sasa hatuna wasiwasi tena na eneo la golikipa, aliyekuwepo mwanzo alikuwa mzuri lakini alikuwa akifanya makosa mengi binafsi labda kwa sababu alicheza mechi nyingi, Hanington katuonyesha kuwa ana kitu flani kizuri nasi tutamsapoti, hatuna kauli nyingine zaidi ya hii asante Hanington  tumekuelewa” walisema.
Huu ulikuwa mchezo wa kwanza kwa Hanington kuitumikia City katika msimu kufuatia kuchelewa kufika kwa kibali chake cha kucheza soka nchini akitokea kwao Uganda licha ya usajili wake kukamilika mapema.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video