MAAFANDE wa Tanzania Prisons wametamba kutowahofia
Yanga katika mechi yao ya ligi kuu Tanzania bara itayopigwa uwanja wa CCM
Sokoine, Mbeya alhamisi februari 19 mwaka huu.
Kocha mkuu wa Prisons, David Mwamwaja amesema
waliweka kambi Dar es salaam wakijua watacheza na Azam fc jumapili ya wiki hii,
lakini wamepata taarifa mapema leo kuwa watakuwa na mchezo dhidi ya Yanga,
uwanja wa Sokoine Alhamisi ya wiki hii, hivyo wamelazimika kusafiri haraka
kurudi Mbeya.
“Timu ilikuwa Dar es salaam, imesafiri leo na
imeingia jioni hii Mbeya. Tunajipanga kwa ajili ya Yanga. Tulifika huko Dar es
salaam kwaajili ya mchezo dhidi ya Azam, lakini tulipoambiwa tunacheza na Yanga
Sokoine Mbeya ikabidi tuje Mbeya leo”. Amesema Mwamwaja.
Kuhusu mechi yenyewe, Mwamwaja amesema: “Tunaifahamu
Yanga, na wao wanatufahamu vizuri, hawawezi kutubeza. Tuko nyumbani lazima
tupambane kupata ushindi, tumepata sare nyingi lakini ni bora kuliko kupoteza. Mimi
bunduki zangu zipo sawa, nitatumia vijana wa chini ya miaka 20
nikiwachanganya na kaka zao”.

0 comments:
Post a Comment