
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Yanga SC ikifanikiwa kuing'oa BDF XI FC katika hatua ya awali ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, itamenyana na mshindi kati ya Sopaka FC ya Kenya na FC Platinum ya Zimbabwe.
Hata hivyo, Afrika Mashariki imeonesha dalili mbaya baada ya mechi za kwanza za michuano ya kimataifa mwishoni mwa wiki, Sofapaka wakipokea kichapo nyumbani cha mabao 2-1 dhidi ya Platinumz na kujiweka katika mazingira magumu ya kufuzu wakiwa ugenini kwa 'Rais asiyetishwa na wazungu', Robert Mugabe nchini Zimbabwe wiki ijayo.
FC Platinum iliandika ushindi huo wa kwenye Uwanja wa Taifa wa Nyayo jijini Nairobi, Kenya jana, mabao yakifungwa na Brian Muzondiwa dakika ya 25 kabla ya Mrundi Fiston Abdoul Razak. kufunga la la kufutia machozi dakika ya 47.
Goli la ushindi la wageni lilifungwa na Donald Ngoma dakika ya 74 na kumfanya kocha mkuu wa Platinum, Norman Mapeza aweke wazi kuwa kikosi chake kilikuwa na bahati kwani kimeanza mazoezi wiki nne tu zilizopita kabla ya mechi hiyo.
"Ndiyo tumeshinda, lakini tunapaswa kufanya mazoezi kwa nguvu zaidi. Tumejiandaa kwa wiki nne tu kwa ajili ya mechi hii, wachezaji wangu katika kipindi hiki bado hawako fiti. Ninafikiri ni kwa sababu ndiyo tunatoka mapumziko ya msimu," amekaririwa kocha huyo na mtandao wa Futaa.com wa Kenya.
"Lengo letu ni kufika mbali zaidi, si kuifunga tu Sofapaka halafu tutolewe katika hatua inayofuata. Tuna lengo la kufika hatu ya makundi. Hii itakuwa hatua nzuri kwetu," amesema zaidi kocha huyo.

0 comments:
Post a Comment