
Baada ya kufanikiwa kuirejesha Ligi Kuu timu yake, Kocha Mkuu wa Mwadui FC, Jamhuri Kiwhelo 'Julio' ametamba kuwa yeye ni KOCHA FUNDI.
Baada ya miaka 27 bila kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, Mwadui FC imefanikiwa kurejea Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kutokana na kumaliza nafasi ya kwanza katika Kundi B la Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu huu.
Mwadui FC imemaliza kileleni mwa msimamo wa Kundi B ikiwa na pointi 46 ikifuatwa na Toto Africans yenye pointi 45 na Oljoro JKT yenye pointi 45 katika nafasi za pili na tatu.
Akiwa Shinyanga leo asubuhi, Julio amesema: "Mimi ni kocha fundi, nimepanda Ligi Kuu na ninakuja kupambana. Siji kushiriki ligi."
"Msimu ujao hakuna cha Yanga, Simba wala Azam. Nitamaliza katika nafasi tatu za juu. Tuna timu nzuri na uongozi imara. Tunashukuru sapoti ambayo trumeipata kutoka uongozi wa mkoa wa Shinyanga na Chama cha Soka mkoani hapa.
"Kama Mungu kapanga, kapanga tu. Tulianza kwa kusuasua dhidi ya Panone FC, Toto Africans na Oljoro JKT, lakini badaye tukawa tunashinda tu. Msimu uliopita tulifanya vizuri na kupanda Ligi Kuu, lakini Mungu hakupanga, tukaondolewa kwa maamuzi ya wakubwa wa soka.
"Sasa tumepanda Ligi Kuu, makubwa yanakuja. Ukisikia mtu anaoa ujue kajipanga maana baada ya kufunga ndoa kuna watoto na ada za shule. Kupanda kwetu Ligi Kuu ni sawa na kuoa, tumejopanga kupambana.
"Toto ilitusumbua sana maana tulikuwa tunabadilishana nayo kukaa kileleni mwa msimamo," amesema zaidi kocha huyo wa zamani wa Tanzania Stars na Simba SC ambaye ameshaapa kamwe hawezi kurejea Simba SC ikiwa chini ya viongozi walioko madarakani kwa sasa.
Mwadui FC yenye maskani yake kwenye Migodi ya Almasi ya Mwadui mkoani Shinyanga, imeungana na timu nyingine tatu; Toto Africans ya Mwanza, Africans Sports ya Tanga na Majimaji FC ya Ruvuma kupanga VPL msimu ujao. Timu zote nne ziliwahi kushiriki ligi hiyo.
Timu mbili zitakazomaliza nafasi za chini VPL msimu huu, zitashuka daraja kuzipisha timu hizo nne, hivyo kuiongeza idadi ya timu ligi kuu kutoka 14 hadi 16.
MSIMAMO KUNDI B BAADA YA MECHI ZA MWISHO JANA
Pos Team Pld W T L Goals Diff Pts
1 • Mwadui 22 13 7 2 40 23 46
2 ↑ Toto African 22 14 3 5 36 18 45
3 ↓ JKT Oljoro 22 13 5 4 34 15 44
4 • Polisi Tabora 22 11 5 6 18 6 38
5 • Geita 22 8 5 9 22 -1 29
6 • Panone 22 6 10 6 16 -1 28
7 • Kanembwa JKT 22 7 6 9 12 -14 27
8 • Rhino Rangers 22 6 7 9 14 -7 25
9 • Polisi Mara 22 5 9 8 21 -8 24
10 • Bukinafaso 22 4 10 8 26 6 22
11 • Polisi Dodoma 22 4 6 12 12 -15 18
12 • Green Warriors 22 2 5 15 18 -22 11

0 comments:
Post a Comment