Tuesday, February 10, 2015

IMG-20150210-WA0048
Kikosi cha Mwadui FC kilichoanza leo
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Kikosi cha Toto Africans ya Mwanza kimeokolewa na Jeshi la Polisi baada ya kuibuka vurugu kubwa katika mechi yao ya raundi ya 21 ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL) dhidi ya Geita FC mjini Geita leo jioni.
Vurugu hizo kwa mujibu wa John Tegete, kocha mkuu wa Toto Africans FC, zimeanza kutokea katika robo saa ya mechi hiyo baada ya refa kuamuru penalti ipigwe dhidi ya wenyeji.
“Baada ya refa kuamua penalti dakiika ya 14, wachezaji wa Geita FC waligomea na kuanza kumshambulia, baadaye mashabiki wakavamia uwanja na kuanza kutushambulia, mawe pia yamerushwa saana uwanjani,” amesema Tegete.
TOTO WASINDIKIZWA NA POLISI 
Baba huyo wa mshambuliaji wa Yanga SC, Jeryson Tegete, amesema wamelazimika kuondoka uwanjani hapo kwa msaada wa Jeshi la Polisi kupitia kikosi chake cha kutuliza ghasia (FFU).

Kikosi cha Toto kimesindikizwa na ‘defender’ tatu kutoka Geita hadi jijini Mwanza.
POINTI 3 MABAO 3
Kwa vurugu hizo, ni wazi kwamba Geita FC itaadhibiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kupokwa pointi zote tatu.

Kanuni za FDL zinaweka wazi kwamba timu inayofanya vurugu inaadhibiwa na timu pinzani inapewa pointi tatu na mabao matatu.
IMG-20150210-WA0046
Mashabiki waliofurika katika uwanja wa Mwadui
MWADUI FC 2-0 POLISI TABORA
Katika mechi nyingine ya Kundi B, Mwadui FC wameifunga Polisi Tabora mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Mwadui, Shinyanga.
Mabao ya timu hiyo inayonolewa na kocha wa zamani wa Simba SC, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ yamefungwa na Bakari Kibodeko katika nusu saa ya mchezo na Kelvin Kongwe dakika ya 38.
Kwa ushindi huo, Mwadui FC inaendelea kuongoza Kundi B ikiwa na pointi 43, nne mbele ya Toto Africans walioko nafasi ya tatu ambao ni wazi watapewa pointi tatu na TFF na kufikisha pointi 42. 
RHINO 1-0 OLJORO
Kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, wageni Oljoro JKT kutoka Arusha wamelifanya Kundi B kuwa gumu baada ya kuwachapa wenyeji Rhino Rangers bao 1-0 leo jioni.

Kwa ushindi huo, Oljoro JKT imepanda hadi nafasi ya pili ikiwa na pointi 41, ikisubiri hatma ya mechi ya Toto Afrikcans dhidi ya Geita FC.
Mwadui FC na Oljoro JKT zimebakisha mechi moja kila moja. Mwadui itamaliza na Burkina Faso ya Morogoro mjini Shinyanga wakati Oljoro itamaliza kwa kuivaa Polisi Tabora mjini Tabora.
POLISI DOM 3-0 GREEN WORRIORS
Kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Polisi Dodoma imeilaza Green Warriors ya Dar es Salaam kwa mabao 3-0.

KANEMBWA 5-0 BURKINA FASO 
Maafande wa JKT Kanembwa wametoa kipigo cha wiki kwa kumpiga ‘mkono’ (5-0) Burkina Faso kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro leo jioni.

PANONE 1-1 POLISI MARA  
Mechi nyingine ya leo ya Kundi B la FDL imeshuhudiwa Panone FC ya Kilimanjaro ikishikwa kwa sare ya 1-1 dhidi ya Polisi Mara kwenye Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video