Tuesday, February 10, 2015

HERM5672-1
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Azam FC itakutana na Mtibwa Sugar FC katika mechi ya visasi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) Uwanja wa Azam jijini Dar es Salaam kesho.
Kikosi cha Mcameroon Joseph Omog kinahitaji ushindi katika mechi hiyo ya raundi ya tisa iliyopaswa kuchezwa Januari 3, ili kirejee kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kufikisha pointi 25 sawa na vinara wa sasa, Yanga SC.
Mtibwa Sugar inayonolewa na nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Mecky Mexime itaingia Uwanja wa Azam FC kesho ikisaka ushindi wake wa kwanza baada ya kucheza mechi saba bila ushindi ikitoka sare mara tano na kupoteza mechi mbili dhidi ya JKT Ruvu na
Kuelekea mechi hiyo, Mexime amesema: “Tulijisahau na kufanya makosa machache ambayo yalitugharimu dhidi ya Yanga, tumesahau yaliyopita na kuanza kujipanga dhidi ya Azam FC. Jambo njema kwetu hatuna majeruhi.”
“Tunahitaji kuwa na mipango mizuri katika kumalizia nafasi tunazozitengeneza. Tulitengeza nafasi nyingi katika mechi iliyopita lakini hatukuwa wazuri katika kuzitumia,” amesema zaidi nahodha huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar FC.
Meneja wa timu ya Azam, Jemedari Said alisema jana kuwa kikosi chao kilichoambulia sare ugenini mjini Morogoro dhidi ya Polisi Moro Jumamosi, kiko vizuri ana anaamini kinashinda leo na kuwang’oa Yanga kileleni.
Mtibwa Sugar, ambayo haina historia nzuri inapokutana na Azam FC jijini Dar es Salaam, iliwang’oa kwa matuta 7-6 matajiri hao katika hatua ya robo-fainali ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar Januari 8 baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1 katika muda wa kawaida wa dakika 90.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video