
KOCHA mkuu wa Simba SC, Goran Kopunovic
anafurahishwa na kiwango cha mshambuliaji wake, Raia wa Uganda, Danny
Sserunkuma ambaye siku za karibuni amekuwa na makali ya kufumania nyavu.
Sserunkuma alifunga bao moja katika ushindi wa
Simba wa mabao 2-0 dhidi ya Ndanda fc huko Nangwanda Sijaona na mabao mawili
katika ushindi wa 2-1 dhidi ya JKT Ruvu uwanja wa Taifa.
“Danny ni mtu anayevutia, nilikutananaye kwa mara
ya kwanza huko Zanzibar, nadhani kwa kiasi fulani alikuwa na kiwango cha chini,
lakini sasa anakuja. Amesema Kopunovic.
“ Unajua nafasi anayocheza Danny ndio nilikuwa
nacheza katika maisha yangu ya soka na nawaelewa vizuri washambuliaji, wakati
wote kitu muhimu ni magoli. Danny ni mtu wa kigeni, ni mchezaji wa kimataifa,
anatoka timu ya taifa ya Uganda, ana uzoefu wa kucheza nje ya Uganda, alicheza
Kenya katika klabu ya Gor Mahia,kwahiyo ni mchezaji muhimu katika timu” Ameongeza
Kopunovic.
Mserbia huyo alipoulizwa kuhusu mwenendo wa klabu
yake katika mechi za ligi kuu Tanzania bara na anajisikiaje kupata matokeo
yasiyoridhisha, amejibu: “Siku zote
nasema ukweli, siku zote kocha Goran anaangalia mechi ijayo, mimi ni mpaganaji
ninayetafuta mafanikio ya timu. Simba ni timu kubwa, inaungwa mkono sana, ina
mashabiki wengi, nina furaha sana kwasababu mashabiki wako upande wangu, ni
watu muhimu sana”. Amesema Kopunovic.
Kumekuwa na madai kuwa wachezaji wa Tanzania
wanashindwa kuwaelewa makocha wa Kizungu, lakini Kopunovic amesema wachezaji wa
Simba wanamuelewa vizuri.
“Nadhani ndiyo, mara zote naongea na wachezaji
wangu kabla na baada ya mechi, maswali yote nayaelekeza kwa wachezaji kuhusu
mazoezi, mfumo wangu, falsafa yangu na mapaka sasa hakuna mtu anayeniambia kuwa
kocha tuna matatizo, hiki sio kitu kizuri kwetu, hiki ni kigumu, nadhani
tunaenda vizuri”.
Simba imeshuka dimbani mara 13, imeshinda 3,
imetoa sare 8 na imefungwa mechi 2 na
kutokana na matokeo hayo ipo nafasi ya 9 nyuma ya Kagera Sugar, Coastal Union,
Mtibwa Sugar na Ruvu Shootings.
Mwishoni mwa wiki hii, Simba wataikabili Polisi
Morogoro katika mechi ya ligi kuu itayopigwa uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.
0 comments:
Post a Comment