Thursday, February 19, 2015


Bahanuzi wakati akiichezea timu yake ya Yanga kabla ya kupelekwa kwa mkopo Polisi Morogoro

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam 

BAADA ya kulamba tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, mshambuliaji Said Bahanunzi wa Polisi Moro FC amesema kusugua benchi kwa muda mrefu katika kikosi cha Yanga SC, kulishusha kiwango chake.

Aidha, mchezaji huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar FC, amesema hatakuwa tayari kubaki katika kikosi cha wanajangwani endapo ataendelea kusugulishwa benchi bila sababu za msingi. 

Bahanunzi, mfungaji bora wa Kombe la Kagame la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, ameibuka mchezaji bora wa mwezi Januari wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kufunga mabao mawili muhimu katika mechi mbilim dhidi ya Ndanda FC na Mbeya City FC yaliyoipaisha timu yake hadi nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo mwezi uliopita.

"Mafanikio yangu yametokana na kupangwa mara kwa mara katika kikosi cha Polisi Moro. Ninashukru kwa kutwaa tuzo. Sikupata nafasi ya kucheza kwa muda mrefu Yanga, lakini hapa ninapewa nafasi na ninashukuru Mungu kwa hilo.

"Bado nina mkataba na Yanga, nitarudi Yanga kwa sababu nina mkataba nao wa muda mrefu. Ligi itakapomalizika, nitazungumza na viongozi vizuri, lakini siko tayari kukaa benchi," amesema zaidi Bahanunzi.

Mshambuliaji huyo amesema hatabaki Yanga SC ikiwa ataendelea kusugulishwa benchi.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video