Friday, February 20, 2015

LIGI kuu Tanzania bara inatarajia kuendelea kesho kwa mechi kadhaa kupigwa viwanja mbalimbali nchini.
Kagera Sugar watakuwa nyumbani uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga kuchuana na Polisi Morogoro.
Kagera wataingia kwenye mechi hiyo wakiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa goli 1-0 dhidi ya JKT Ruvu mwishoni mwa wiki iliyopita uwanja huo, wakati Polisi wao walifungwa 2-0 na Simba uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Mechi nyingine itawakutanisha Ndanda fc dhidi ya Coastal Union uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Ndanda fc mwishoni mwa wiki iliyopita walitoka suluhu na Mtibwa Sugar uwanja wa nyumbani, wakati Coastal nao walitoka suluhu na Mbeya City fc uwanja wa Mkwakwani.
Mgambo JKT wataikaribisha Mtibwa uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Jumapili, Februari 22, Simba watakuwa ugenini CCM Kambarage kupepetana na Stand United, wakati Mbeya City fc wataikaribisha Yanga uwanja wa Sokoine.
Usiku Azam fc watashuka dimbani kuchuana na Tanzania Prisons.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video