
MASHETANI Wekundu, Manchester United leo wapo ugenini kukabiliana na West Ham United katika mechi ya ligi kuu soka nchini England itayoanza majira ya saa 1:15 usiku.
Katika mechi ya leo, Louis van Gaal anatarajia kuwachezesha Robin van Persie na Radamel Falcao katika safu ya ushambuliaji na hii inamaanisha Wayne Rooney atachezeshwa kama kiungo wa katikati.
Mechi nyingine za leo ni Burnley dhidi ya West Brom itayoanza mapema saa 9:00 alasiri, wakati Newcastle watakuwa nyumbani kuchuana na Stoke kuanzia majira ya 11:00 jioni.
0 comments:
Post a Comment