Sunday, February 8, 2015

HERM5672-1
Na Richard Bakana
Na Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara, Azam FC, jana wamejikuta wakigawana pointi  na Polisi Moro baada ya kutoa sare ya bao 2-2 katika mtanange uliopigwa uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro.
Azam walijipatia bao la kwanza kupitia kwa Kipre Tchetche katika dakika ya 12 ya mchezo huo baada ya kupiga shuti kali ambalo lilimbabatiza beki wa Polisi Morogoro na kumuacha kipa Tony Kavishe akiwa hana cha kufanya na jitihada zake za kuokoa bao hilo kugonga mwamba.
Dakika ya 29 Polisi Moro walisawazisha bao kupitia Edward Christopher baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira wa kona ambao ulimbabatiza kiungo wa Azam FC, Frank Domayo na kurudi ndani lakini tayari alikuwa amevuka mstari wa langoni na muamuzi Judithia kuamuru bao.
Katika dakika ya 29 Polisi Moro walifanya mabadiliko na Lolanga mapunda akatoka na nafasi yake ikachukuliwa na Nahoda Bakar ambaye kwa kiasi chake aliisaidia timu yake kupeleka mashambulizi katika lango la Azam FC.
Kunako dakika ya 43 Mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche alizawadiwa kadi ya Njano baada ya kulalamika akipinga maamuzi ya refa alipompulizia kipyenga cha kuibia yaani offside alipokuwa akielekea langoni mwa wenyeji wao.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu zote zikiwa na bao moja moja, tayari wachezaji wa wili wa Azam akiwemo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ walikuwa wamepewa kadi za njano huku Polisi moro wakionekana kucheza bila madhambi.
Baada ya kipindi cha pili kuanza katika dakika ya 47 Said Bahanuzi alikosa bao la wazi baada ya kuwaacha mabeki wa Azam FC na kupiga shuti kali ambalo lilikosa mmaliziaji.
Kocha Joseph Omog dakika ya 50, aliamua kumpumzisha winga Brian Majwega na nafasi yake kuchukuliwa na John Bocco ‘Adebayo’ ambapo kunako dakika ya 58 mshambuliaji huyo alikosa bao la wazi baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Didier Kavumbagu alipopiga mpira na kuupaisha juu.
Ili kuhakikisha Azam wanasaka pointi tatu, Omog alimpumzisha Domayo katika dakika ya 60 na nafasi yake kuchukuliwa na Mudathiri Yahya lakini bado mambo hayakutosha kutimiza dhamira ya kuibuka washindi katika uwanja wa ugenini.
Kunako dakika ya 68 Muivory Coat mwingine wa Azam FC , Michael Bolou aliiandikia timu yake bao la pili kufatia mpira wa adhabu ndogo ya free kick ambapo mpira huo ulimgonga Nahoda Bakar na kuingia langoni.
Polisi Moro baada ya kutokata tamaa walijikuta wakipata bao la kusawazisha kupitia kwa Selemani Kassim Silembe akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona ikiwa ni dakika ya 80 ya kipindi cha pili ikiwa ni uzembe wa mabeki wa Azam ambao walimuacha akiruka juu pekee.
Dakika ya 87 muamuzi Judithia alimzawadia kadi ya njano Edward Christopher baada ya kumfanyia madhambi beki wa Azam FC, Shomari Kapombe.
Ili kuangalia labda wataweza kupata pointi tatu katika mchezo huo Kocha Omog, aliamua kumpumzisha Kipre Tchetche kunako dakika ya 89 na nafasi yake kuchukuliwa na Kelvin Friday.
Hadi dakika ya mwisho Wanalamba lamba hao kutoka Chamazi pamoja na Askari polisi hao wa Morogoro walijikuta wakitoshana nguvu kwa kufungana bao 2 kwa 2.
Kutokana na matokeo hayo Azam FC sasa wanakuwa wamefikisha pointi 22 sawa na Yanga huku akikabiliwa na mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar wiki kesho kabla ya kuwavaa El Merreikh katika michuano ya klabu bingwa Afrika.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video