
Rais wa Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Bw Jamal Malinzi ametuma salama za pongezi kwa Rais Sidy Diallo wa Shirikisho la soka nchini Ivory Coast (FIF) kwa kutwaa Ubingwa wa Mataifa Afrika.
Katika salam zake Bw. Malinzi amesema mafanikio hayo ya kutwaa Ubingwa wa Afrika yametokana na juhudi za Rais huyo pamoja na Kamati yake ya Utendaji.
“Kwa niaba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), familia ya mpira na watanzania kwa ujumla wanawapa pongezi Shirikisho la mpira wa Miguu la Ivory Coast kwa kutwaa Ubingwa huo wa Afrika kwa mara pili” Imesema taarifa iliyotumwa na Ofisa habari wa TFF Baraka Kizuguto.
0 comments:
Post a Comment