
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Ule mgogoro wa Azam TV na SuperSport kuhusu haki za matangazo ya televisheni ya Ligi Kuu ya Uganda (UPL), bado unaendelea na safari hii umetinga mahakamani.
Amri ya mahakama kusitisha matangazo yoyote ya moja kwa moja na kurekodi kwa televisheni ya UPL imetoka ikiwahusu Azam TV walionunua haki za matangazo ya ligi hiyo wiki iliyopita.
Taarifa iliyochapwa kwenye mtandao rasmi wa Shirikisho la Soka la Uganda (FUFA) imeeleza kuwa hatua hiyo ni kutokana na amri ya Mahakama Kuu ya Uganda iliyotolewa Ijumaa 13 Februari 2015 ikieleza kuwa ligi hiyo haipaswi kutangazwa moja kwa moja wala kurekodiwa na kituo chochote cha Tv hadi Jumanne 3 Machi 2015.
HAKUNA TV KUREKODI
Ili kutomaliza utamu, soma mwenye taarifa hiyo hapo chini ya FUFA:-
"On 13th February and 16th February 2015, the matter came before civil court and the decision has been made to extend the hearing and subsequent restrictive order to Tuesday, 3rd March 2015. Basing on that, and in consideration of the consequences that may arise, all stake holders are hereby informed that no Television recording and relaying of live match broadcast should be made during the period up to 3rd March 2015 when a court decision is made on the matter,
The UPL secretariat, UPL Clubs and match officials are instructed NOT to allow Television recording and broadcast. However, the fixture and matches will be played as scheduled, since the court order does not stop in any way the playing of these matches accordingly."
Taarifa hiyo imesainiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa FUFA, Edgar Watson.
Mzunguko wa pili wa UPL ulianza jana Jumanne 17 Februari 2015 bila ligi hiyo kuonekana kwenye Tv na kusikika moja kwa moja kwenye redio.
Azam TV walionunua haki za matangazo ya TV ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa Sh. bilioni 5.5, waliinunua pia UPL kwa mabilioni ya fedha siku chache zilizopita.
0 comments:
Post a Comment