Sunday, February 8, 2015

4
Na Richard Bakana
KINDA wa Kitanzania anayeumiza vichwa vya waarabu wa Qatar kwa kiwango chake matata, Martin Tangazi, amezungumzia changamoto zinazomkabili akiwa na timu yake ya Aspire Football Dreams iliyopo Doha, chini ya Aspire Academy (Centre of Excellence) ya mtoto wa Mfalme wa nchi hiyo Hamad bin Khalifa Al Thani.
Akizungumza na Shaffihdauda.com akiwa Qatar, Tangazi ambaye alizaliwa Juni 28, 1997, Amesema kuwa moja kati ya Changamoto alizonazo ugenini hapo ni swala la Ushirikina kwenye michezo ambapo amedai kuwa nchi zinazotoka Afrika Magharibi ndio zinaongoza kwa Imani hiyo huku yeye akimtegemea sana Mungu kwa kila kitu.
“Hapana!, siamini kabisa imani hiyo, ila nisikudanganye wachezaji wengi hapa wanatumia, bora ya kwetu Bongo, amini ninayokwambia, Wanaofanya hivyo ni wachezaji kutoka Afrika Magharibi. Amesema kinda huyo na kuongeza “ Mimi ninaamini katika Mungu, Juhudi na nidhamu tu.”.
 
TANGAZI
Kinda huyu ambaye alikuwa mmoja wa nyota waliounda Kombaini ya Taifa ya Copa Coca Cola chini ya miaka 17, iliyokwenda nchini Afrika Kusini mapema mwaka 2013, ambako yeye alikuwa nahodha wa Tanzania na baada ya kufanya maajabu akachaguliwa kwenye Kombaini ya Afrika nzima ya Copa Coca Cola, amesema kuwa, Waarabu hawajui Ushirikina zaidi ya kumuomba Mungu kila wakati, kitu ambacho kinawafanya wazidi kuwa vizuri tofauti na vijana wa Kiafrika ambao wameendekeza Uchawi na kubweteka.
Nyota huyo wa baadae wa Taifa Stars na Tanzania kwa ujumla ikibidi Dunia nzima, ameenda mbali na kusema kuwa, Soka ya Tanzania inatakiwa ibadilike, timu kama za Simba na Yanga ambazo ndio wakongwe wa ligi kuu VPL, ziachane na Imani hiyo kama kweli wanatumia katika michezo yao ili kukuza Mpira wa Bongo akidai kuwa imani hiyo inafanya Mchezaji anashindwa kujituma uwanjani hata mazoezini akijua kuwa ananguvu za giza.

 
TAGAZI-5
“Hizo ndio zinazochangia kuua soka letu lazima ziachane na mambo ya kishirikina, Wachezaji wakiamini hivyo wanashindwa kutia bidii, Viongozi wabadirike wajue Soka ni Biashara hata wachezaji wanatakiwa kujitambua”  Ameongezea Tangazi ambaye aliifunga FC Barcelona moja ya mabao 2-1 ambayo yalipatikana katika mchezo wa Fainali ya michuano ya Academy kubwa Duniani iliyofanyika nchini Hispania Mei 2014 na Mtanzania huyo kuipa Kikombe hicho timu ya Aspire Football Dreams.

Katika michuano hiyo ambayo iliandaliwa na FC Barcelona na kuziarika timu kubwa kama Real Madrid, Inter Milan, FC Porto, Man City, Espanyola, Valencia, Juventus, Sporting Lisbon na nyingine nyingi, Mtanzania huyo alifanikiwa kuibuka mchezaji bora wa mashindano na kuwaacha Wazungu wakimtolea macho kwa kiwango alichoonyesha ikiwemo umahiri wa kucheka na Nyavu.
TANGAZI 3

Kama hiyo haitoshi, Tangazi ambaye amewahi kuichezea Twalipo Camp ya jijini Dar es salaam kabla hajatimkia Qatar, hivi karibuni amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Academy yao, ambapo anasema kuwa zoezi hilo lilifanyika kwa kushindanisha viwango vya mchezaji mmoja mmoja na Kinda huyo ambaye anamahusiano mazuri na Kiungo wa zamani wa Simba Mwinyi Kazimoto ambaye pia anakipiga nchini humo, aliweza kuwapiga fimbo waarabu na kuibuka kidedea.

 
TANGAZI 4
WASIFU
JINA KAMILI: Martin Ildifonce Tangazi
UMRI: Miaka 17
KUZALIWA: Juni 28, 1997.
ALIKOZALIWA: Morogoro, Tanzania
TIMU: Aspire Academy, Doha Qatar
NAFASI DIMBANI: Kiungo/Mshambuliaji
TIMU ZA ZAMANI: Soba, Twalipo Camp

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video