
MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc wamelazimisha sare ya mabao 2-2 na Polisi Morogoro katika mechi ya ligi kuu iliyopigwa uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro leo jioni.
Kwa matokeo hayo Azam inarejea kileleni kwa pointi 22 sawa na Yanga baada ya kucheza mechi 12, lakini wanalambalamba wanaongeza kwa wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Mechi nyingine ilipigwa uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga ambapo Simba imetoka suluhu (0-0) na wenyeji Coastal Union.
Jijini Dar es salaam, JKT Ruvu wametoka sare ya 1-1 na Mbeya City fc katika mechi ya ligi kuu iliyopigwa uwanja wa Azam Complex.
Ndanda fc ikiwa nyumbani Nagwanda Sijaona imelazimishwa sare ya 1-1 na Stand Unitited ya Shinyanga.
Baada ya kufanya vibaya katika mechi mbili zilizopita uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, Kagera Sugar imeshinda bao 1-0 dhidi ya Mgambo JKT.
Kesho katika uwanja wa Taifa, Yanga watachuana na Mtibwa Sugar.
0 comments:
Post a Comment