Kocha mkuu wa Simba, Goran Kopunovic (kulia) akifurahi na msaidizi wake, Seleman Matola
"Anafanya kazi kwa juhudi, ana kipaji kikubwa, ni kijana mdogo, ni kocha mkubwa, anapenda kujifunza, nadhani atakuja kuwa kocha wa kiwango cha juu zaidi ndani ya klabu ya Simba".
"Viongozi wa Simba watambue hili, Matola ni kijana wao, ni gwiji wa klabu, ana kipaji cha hali ya juu, nikiondoka mimi atakuwa tayari ameiva kuwa kocha mkuu wa Simba".
"Tulikutana naye kwa mara ya kwanza Zanzibar, anafanya kazi nzuri, sitaki aondoke Simba, nahitaji kumuona akiendelea kukua katika kazi ya kufundisha mpira".
Haya ni maneno ya kocha mkuu wa Simba, Goran Kopunovic akimsifia kocha wake msaidizi, kiungo mahiri wa zamani wa Simba, Seleman Matola.
Kopunovic amesema hayo asubuhi hii Simba ikijiandaa kuingia uwanjani jioni ya leo kukabiliana na Stand United kwenye uwanja wa CCM Kambarage.
Matola naye amejibu akisema: "Kopunovic ni kocha mzuri, anapenda kazi yake, anajituma muda wote. Anazungumza vizuri na wachezaji wake, Simba hii ataifikisha mbali. Nampenda sana na tunafanya kazi nzuri".
0 comments:
Post a Comment