Tuesday, February 10, 2015

Al Merreikh
Na Richard Bakana, Dar es salaam
MABINGWA wa Afrika Mashariki na Kati, Kagame Cup, klabu ya Al Merreikh Keshokutwa Februari 12 wanatarajia kutua Jijini Dar es salaam kuwavaa wenyeji wao Azam FC kunako michuano ya klabu Bingwa Afrika mwishoni mwa wiki hii katika Uwanja wa Chamazi.
Akizungumza leo Ofisa habari wa Azam FC, Jafar Idd Maganga, amesema kuwa baada ya kuwasili Nchini, miamba hao kutoka Sudan viongozi wa timu hiyo watakutana na waandishi wa habari katika Ofisi za TFF zilizopo Karume.
Kwa mara ya mwisho Azam na Al Merreikh walikutana katika hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Kagame Nchini Rwanda na Lamba lamba wakatolewa kwa mikwaju ya penati huku Wasudan hao wakisonga mbele na kunyakua Ubingwa wa kombe hilo hapo mwaka jana.
Jafar Idd pia amezungumzia maandalizi ya timu yao kuelekea mchezo wa kesho wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Mtibwa Sugar na kudai kuwa wamejiandaa kwa ushindi licha ya kutambua uwezo wa wapinzani wao.
“Wachezaji wote wanaendelea na mazoezi,  tunatambua utakuwa ni mchezo mgumu lakini kama mabingwa watetezi tumejipanga kupata ushindi, Mtibwa tulikutana nao Mapinduzi wakatutoa kwa penati hivyo tumejipanga zaidi, Hakuna majeruhi kwahiyo ni kazi ya mwalimu yeye ndio anajua atampanga nani” Amesema Jafar Idd Maganga.
Kesho Azam FC watakuwa wamerejea kucheza nyumbani kwao baada ya kukaa nje ya Uwanja wao kwa takribani miezi mitatu kutokana na ziara za nje ya Nchi, Kombe la Mapinduzi na mechi za nje ya jiji la Dar es salaam iliyokuwa ikiwakabiri.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video