
BAADA ya kufuta ukame wa kufunga magoli katika
mechi za ligi kuu, Mshambuliaji wa Simba, Danny Sserunkuma amesema limekuwa
jambo jema kwake kufunga magoli matatu mpaka sasa.
Danny amesema kazi ya mshambuliaji ni kufunga
magoli na inapokuwa kinyume lazima presha iwe kubwa.
“Siku zote ni vizuri kwa mshambuliaji unapoanza
kufunga magoli na kuisaidia timu kupata ushindi, hata nilipokuwa sifungi
nilikuwa na furaha kwasababu timu ilishinda kombe, lakini kwasasa nina furaha
zaidi baada ya kuanza kufunga, kwa
mshambuliaji hili ni jambo nzuri.”Amesema Danny na kuongeza: “Siku zote kuna presha, lakini kocha
anatuambia tufurahie mchezo, tusiwazie presha,
siku zote presha ipo katika soka”.
Wakati huo huo, Emmanuel Okwi amesema anamfahamu
vizuri Danny na amecheza naye timu ya taifa na hana wasiwasi na uwezo wake.
“Namjua Danny (Sserunkuma), ni mfungaji mzuri, Kenya
alifunga sana, kilichomsumbua hapa Tanzania ni kukosa uzoefu na wachezaji
wenzake, ona sasa amepata uzoefu na ameanza kufunga”.
Simba ina wachezaji watano
wa Kigeni wote kutoka Uganda ambao ni Juko Mursheed, Joseph Owino, Danny
Sserunkuma, Emmanuel Okwi na Danny Sserunkuma.
0 comments:
Post a Comment