
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Bodi ya Ligi Kuu nchini (TPLB) imesema mechi ya kusaka bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL) msimu huu itachezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro Ijumaa.
Mechi hiyo itahusisha kinara wa Kundi A (Africans Sports) na kinara wa Kundi B (Mwadui FC), kwa mujibu wa Kanuni za Ligi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) toleo la 2014.
Africans Sports iliyoanzishwa 1936 (sawa na Simba SC), ilipanda Ligi Kuu (kipindi hicho Ligi Daraja la Kwanza) mwaka 1988, ikatwaa taji la Muungano, Coastal Union wakitwaa ubingwa wa Tanzania Bara, lakini Sports ikashuka daraja 1991.
Timu hiyo ya jijini Tanga imerejea tena Ligi Kuu baada ya kumaliza kileleni mwa msimamo wa Kundi A lilokuwa na timu nyingine 13 wakati Mwadui FC imemaliza nafasi ya kwanza Kundi B ambalo pia likuwa na ushindani mkali wa timu 14.
MSIMAMO KUNDI A BAADA YA MECHI ZOTE 22
Pos Team Pld W T L Goals Diff Pts
1 ↑ African Sports 22 15 3 4 28:16 12 48
2 ↓ Majimaji 22 13 6 3 28:14 14 45
3 • Friends Rangers 22 10 8 4 25:18 7 38
4 • Lipuli 22 9 10 3 17:10 7 37
5 • Kimondo 22 9 3 10 21:23 -2 30
6 • Kurugenzi 22 6 9 7 20:21 -1 27
7 • Tessema 22 7 5 10 14:19 -5 26
8 • JKT Mlale 22 6 7 9 20:21 -1 25
9 • Ashanti United 22 6 6 10 26:32 -6 24
10 • African Lyon 22 5 6 11 17:22 -5 21
11 • Villa Squad 22 5 5 12 14:26 -12 20
12 • Polisi Dar 22 3 8 11 18:26 -8 17
MSIMAMO KUNDI A BAADA YA MECHI ZOTE 22
Pos Team Pld W T L Goals Diff Pts
1 • Mwadui 22 13 7 2 40 23 46
2 ↑ Toto African 22 14 3 5 36 18 45
3 ↓ JKT Oljoro 22 13 5 4 34 15 44
4 • Polisi Tabora 22 11 5 6 18 6 38
5 • Geita 22 8 5 9 22 -1 29
6 • Panone 22 6 10 6 16 -1 28
7 • Kanembwa JKT 22 7 6 9 12 -14 27
8 • Rhino Rangers 22 6 7 9 14 -7 25
9 • Polisi Mara 22 5 9 8 21 -8 24
10 • Bukinafaso 22 4 10 8 26 6 22
11 • Polisi Dodoma 22 4 6 12 12 -15 18
12 • Green Warriors 22 2 5 15 18 -22 11

0 comments:
Post a Comment