Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons, David Mwamaja amesema wamelazimishwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kucheza mechi Alhamisi dhidi ya Yanga SC mjini Mbeya.
Mwamaja amesema kikosi chake kilichokuwa kimeweka kambi jijini hapa kujiandaa kwa mechi ya mwishoni mwa wiki hii dhidi ya mabingwa watetezi Azam FC, kimelazimika kurejea jijini Mbeya baada ya kutakiwa kufanya hivyo na TFF.
Amesema kikosi chake kimetua nyumbani, Mbeya leo jioni, tayari kuwavaa Yanga SC ambao wametamba moto wao hauzimiki kwa sasa,
“Timu ilikuwa Dar es salaam tukijiandaa kwa mechi dhidi ya Azam, lakini tumelazimishwa kurejea Dar es Salaam kucheza dhidi ya Yanga," amesema kocha huyo aliyewahi kuinoa Simba SC mwaka 1999 wakati Mtibwa Sugar FC wakitwaa taji la kwanza la Tanzania Bara.
Mwamaja ambaye kikosi chake kiko mkiani mwa msimamo, amesema hana hofu dhidi ya kikosi cha Yanga SC kwa kuwa anakifahamu vyema.
"Yanga tunawajua na wao pia wanajua moto wetu. Tumekuwa na matokeo ya sare nyingi, lakini sare si mbaya, bunduki zetu ziko sawa kwa ajili ya mechi hiyo," amesema zaidi Mwamaja.
MSIMAMO WA VPL KWA SASA
Pos Team Pld W T L Goals Diff Pts
1 • Logo Azam 13 7 4 2 22 10 25
2 • Logo Yanga 13 7 4 2 15 8 25
3 ↑ Logo Kagera 15 5 6 4 12 1 21
4 ↑ Logo Simba 14 4 8 2 15 4 20
5 ↓ Logo Mtibwa 14 4 7 3 15 1 19
6 • Logo Ruvu Stars 14 5 4 5 10 -1 19
7 • Logo Coastal 15 4 7 4 10 1 19
8 ↓ Logo JKT Ruvu 15 5 4 6 14 -1 19
9 ↓ Logo Polisi Moro 15 4 7 4 12 -1 19
10 • Logo Mbeya City 14 4 5 5 9 -2 17
11 • Logo Ndanda 15 4 4 7 13 -5 16
12 • Logo Stand Utd 15 3 6 6 13 -5 15
13 • Logo Mgambo 13 4 2 7 7 -8 14
14 • Logo Prisons 13 1 8 4 10 -2 11

0 comments:
Post a Comment