TIMU ya Kata ya Makorongoni imefanikiwa kubeba kombe la Hepautwa baada ya kuwafunga wapinzani wao wa jadi timu ya Kata ya Kitanzani kwa magoli 3 -0 katika mtanange uliohudhuriwa na mamia ya mashabiki wapenda soka mkoani Iringa katika mchezo uliochezwa uwanja Samora.
Kata ya Makorongoni chini ya mchezaji bora wa mashindano hayo mshambuliaji mwenye uchu wa magoli na kipaji cha pekee David Mhanga (17) alifanikiwa kuipatia magoli mawili lingine likifungwa na Leonard Geka yote yakifungwa kipindi cha pili cha mchezo huo uliokuwa na upinzani tangu kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kusomana mchezo kama ilivyokuwa kipindi cha kwanza na katika dakika. 66 ya kipindi cha pili mchezaji Leonard Geka aliwapatia goli la kwanza kata ya Makorongoni baadaya ya kazi nzuri ya David Mhanga kupiga kichwa kilichookolewa na golikipa wa Kitanzini ndipo shuti kali la mguu wa kulia kutoka kwa Geka lilipotinga kimiani na kuandika goli la kwanza kwa timu yake.
Dakika ya 86 Makorongoni walipata goli la pili na likiwekwa wavuni na David Mhanga aliyekuwa mchezaji bora wa mechi hiyo baada ya kuwapiga chenga mabeki wa Kata ya Kitanzini na kumchanganya kipa wa Kitanzini Abel.

Magoli hayo yaliwavunja nguvu kata ya Makorongoni na dakika ya 90 alikuwa David Mhanga tena aliyewahakikishia Makorongoni ubingwa wa kwanza wa mashindano ya Kombe la Hepautwa kwa kufunga goli la tatu na ushindi katika fainali hiyo.
Kwa ushindi huo timu ya Makorongoni imefanikiwa kujinyakulia kitita cha shilingi 1,000,000 na kombe , mshindi wa pili timu ya Kata ya Kitanzini walijipatia shilingi 600,000 na mshindi wa tatu kata ya Kihesa aliondoka na shilingi 300,000.
Mdhamini wa mashindano hayo Nuru Hepautwa akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi alizishukuru kata zote kwa kushiriki na kuahidi mwakani kuyaboresha zaidi katika vipengele vya zawadi na kuwataka wachezaji kujituma zaidi kutumia michezo kama ajira itakayowakomboa katika umaskini.

0 comments:
Post a Comment