KESI inayomhusu mshambuliaji, Mganda Emmanuel Okwi
inasikilizwa muda huu na kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji ya Shirikisho
la Soka Tanzania.
Habari za ndani zinaeleza kuwa mvutano wa kisheria
ni mkali kuhusu kesi hiyo inayosikilizwa katika Hoteli ya Colosseum iliyopo
jijini Dar es salaam.
Hata hivyo inasemekana maamuzi yatafikiwa leo hii
kama mvutano huo utafikia tamati.
Okwi alisaini mkataba mfupi wa miezi sita na klabu
ya Simba kwa madai ya kulinda kiwango chake wakati ikiwa na kesi na klabu yake
ya Yanga.
Lakini uongozi wa Yanga unadai nyota huyo
aliyeichezea Simba jana katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia ni
mchezaji wao na amebakiza mkataba wa miaka miwili.
Baada ya kuona Okwi amesaini mkataba na Simba,
Yanga walichokifanya ni kuandika barua TFF juu ya suala hilo na kuomba kulipwa
fidia ya US Dollar 500,000 (sawa na TZS 800,000,000/=) kutoka kwa klabu
ya Simba, wakala wake na mchezaji mwenyewe aliongeza.
0 comments:
Post a Comment