Na
Baraka Mpenja, Dar es salaam
0712461976
0712461976
YANGA
SC chini ya kocha Mbrazil, Marcio Maximo ilitarajia kucheza mechi ya mwisho ya
kimataifa ya kirafiki dhidi ya Big
Bullets (zamani Bata Bullets) ya Malawi leo
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kufikia
jana usiku, uongozi wa Yanga kupitia kwa Afisa habari wake, Baraka Kizuguto
ulikaririwa na vyombo vya habari kuwa maandalizi kwa ajili ya mechi hiyo
yamekamilika kwa mujibu wa waandaaji DRFA.
Kwa tafsiri
ya haraka haraka tayari Yanga walikuwa wanawasiliana na chama cha soka cha mkoa
wa Dar es salaam, DRFA, kuhusu ujio wa Big Bullets na ndio maana Kizuguto
alisema kila kitu kinakwenda sawa na kuwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi
leo.
Mpaka
kufikia mapema leo asubuhi, mashabiki walitambua uwepo wa mechi hiyo, lakini
ghafla taarifa kutoka Yanga zinaeleza kuwa mchezo huo haupo tena kwasababu
Wamalawi hawajawasili nchini.
Taarifa
ya Yanga katika ukurasa rasmi wa mtandao wa kijamii imesomeka:
“KUMRADHI:
Wapenzi, wanachama, washabiki na wadau wa soka kwa ujumla, mechi kati ya Young
Africans dhidi ya Big Bullets iliyokua ifanyike leo haitakuwepo.
Kwa mujibu wa waandaji wa mchezo huo DRFA timu ya Big Bullets imeshindwa
kuwasili nchini, na jitihada za kupata timu nyingine imeshindikana.
Tunawaomba
radhi kwa usumbufu wote ambao umejitokeza.
Daima Mbele Nyuma Mwiko”.
Kutokana na suala hilo, binafsi kuna baadhi ya mambo nimeona ni
vyema kuyasema ili yasijirudie tena;
Mosi; ucheleweshaji wa taarifa kwa mambo muhimu kama mechi ya
leo ni kuwakosea haki wapenzi na wadau wa soka.
Kwanini mpaka kufikia jana usiku DRFA wasijue kama Big Bullets
hawaji nchini?, labda kama waliwaambia watakuja siku hiyo hiyo ya mechi.
Lakini hata kama ni hivyo, kwanini hawakuthibitisha kama usafiri
wa uhakika upo kwa Big Bullets kufikia jana?
Zikiwa zimesalia takribani saa tano kuanza kwa mechi, taarifa
kama hii inatoka, kweli ni uungwana?
Sikatai, yawezekana ni sababu zilizo nje ya uwezo wa kibinadamu,
lakini kwa watu wenye kujua majukumu yao vizuri walitakiwa kujua mpaka kufikia
jana.
Najaribu kujenga hoja ya kuleta usumbufu mkubwa, Fikiria muda
huu mtu anatoka mikao ya jirani, Tanga, Morogoro, Pwani kuja kuangalia mechi,
halafu kwa bahati mbaya hana chanzo cha habari, anatua Ubungo wanamwambia mechi
haipo. Ni haki kwake?
Kwa hili DRF wamechemsha, wala hakuna haja ya kupepesa macho.
Siku nyingine wajipange.
Mechi kubwa kama hii inatakiwa timu pinzani iwepo siku moja au
mbili kabla. Mambo ya siku ya mechi ni usanii tu.
Kama watu walishakata tiketi kabisa itakuwaje? Watarudishiwa kwasababu
hakuna uhakika wa mechi nyingine? Au ndio moja kwa moja?
Hakika kuna mambo yanayotakiwa kupigwa vita kama ubabaishaji
huu.
DRA kama waandaaji, lawama zote mnabeba ninyi na kwa sehemu Fulani
Yanga.
Pili; Viongozi wa Yanga wanatakiwa kuwa makini kufuatilia taarifa
muhimu kuhusu klabu yao.
Yawezekana DRFA wamewaangusha kwasababu wao ndio walikuwa na
dhamana ya mechi hiyo, lakini kama wahusika wakuu walitakiwa kufuatilia kwa
ukaribu zaidi kwa manufaa ya mashabiki wao.
Inawezekana DRFA wakachukiwa na wapenzi wa Yanga, lakini hata
viongozi wao wanatakiwa kubeba sehemu ya lawama hizo.
Kwanini mpaka kufikia jana walikuwa hawana uhakika na
wakawatangazia mashabiki wao kuwa mechi ipo? Hapa walitakiwa kuwa watulivu na
kuulizia mara kwa mara ili kutoa taarifa rasmi jana.
Kwa bahati mbaya sana kuna baadhi ya viongozi walikaririwa
wakisema Big Bullets imewasili nchini, lakini kumbe hawajui kitu.
Sawa na tamasha la ‘Coastal Day’ leo hii septemba 7, makamu
mwenyekiti wa Coastal alikaririwa jana akisema hajui chochote kuhusu siku hiyo.
Kama kiongozi wa juu hajui siku kama hiyo, unadhani kuna uongozi
hapo? Taarifa jambo jema sana jamani.
Ni kweli Yanga na DRFA walikuwa na mawasiliano ya mara kwa mara
mpaka kufikia jana?
Sijui, lakini kwa haya yaliyojitokeza, kuna shaka juu
ya hilo
0 comments:
Post a Comment