
Mapumziko: Kiungo wa Manchester City, Samir Nasri akiwa likizo huko Ibiza na demu wake Anara Atanes
KIUNGO wa Manchester City, Samir Nasri ameamua kuitumia likizo yake fupi ya kupisha mechi za kimataifa kwa kula bata na mpenzi wake Anara Atanes huko Ibiza.
Nyota huyo mwenye miaka 27 aliamua kujiondoa mwenyewe katika uwezekano wa kuitwa katika kikosi cha Ufaransa chini ya kocha Didier Deschamps baada ya utata uliojitokeza kufuatia kuachwa katika kikosi cha fainali za kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
Demu wa Nasri alimtukana matusi ya nguoni Deschamps mwezi mei mwaka huu baada ya kumuacha basha wake katika kikosi cha Ufaransa.
Mwanamke huyo aliandika katika mtandao wa Twita: 'F*** france and f*** Deschamps! What a s*** manager! (Hatujaona haja ya kutafsiri kwa sababu za kimaadili)

Likizo fupi: Nasri akipozi katika picha na demu wake Atanes na Carla Dona Garcia (kulia) katika ziara yao ya Ibiza
0 comments:
Post a Comment