
BAO pekee la Musa Hassan Mgosi limeipa Mtibwa
Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya Ndanda fc katika mchezo wa kirafiki uliopigwa jioni
ya leo uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Msemaji wa Mtibwa Sugar, Tobias Kifaru
Ligalambwike amesema Mgosi alifunga bao hilo kipindi cha pili kwa shuti kali.
Licha ya kufungwa, Kifaru alisema Ndanda walijitahidi
kucheza soka safi, lakini walizidiwa maarifa na mabingwa hao wa mwaka 1999 na
2000.
Kifaru aliongeza kuwa Mtibwa ni timu kubwa na ndio maana Simba
waliikimbia na kucheza na timu dhaifu ya Gor Mahia ambayo waliishinda mabao 3-0
jana uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment