
Mcheza bora wa dunia: EA Sports wamemuweka nyota wa Barcelona, Lionel Messi kuwa namba moja katika michezo mipya ya FIFA 15
CRISTIANO Ronaldo alimgaragaza Lionel Messi katika tuzo ya Ballon d'Or mapema mwaka huu,lakini nyota huyo wa Barcelona amelipa kisasi kwa mpinzani wake huyo mkubwa kwa kushinda tuzo nyingine.
Akiwa amepata pointi 93 kati ya 100, messi amekuwa namba moja katika tuzo ya michezo ya Video ya FIFA, (FIFA 15) ambayo itatangazwa rasmi septemba 26 mwaka huu huko UK.
Ili kuwapa nafasi mashabiki kupiga kura kabla, waendeshaji wa tuzo hiyo, EA Sports walitangaza majina ya wachezaji 50.

Mtu anayetakiwa: Barcelona watakuwa maarufu zaidi katika michezo mipya ya Video baada ya Messi kuibuka kinara kwa takwimu za sasa.

Namba mbili: Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amepewa pointi 92 katika tuzo ya FIFA 15

Hatari: EA Sports wameupa uwezo wa Ronaldo wa kupiga mashuti pointi 93 kati ya 100.
Messi amemshinda Ronaldo kwa tofauti ya pointi moja nyota wa Real Madrid aliyepata alama 92 hasa katika uwezo wa kufunga mabao.
Nyota wa Bayern Munich na Uholanzi Arjen Robben ameshika namba tatu kwa pointi zake 90.
Takwimu hizo zinazozingatia zaidi kiwango cha mchezaji katika mechi za ligi na makombe katika siku 365 zilizopita, zinaonesga uwezo wa kila mchezaji kila anapotumika katika mechi.
Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Zlatan Ibrahimovic na kipa wa Bayern Munich, Manuel Neuer wameshika nafasi ya nne na tano, licha ya kupata pointi sawa na Robben.
Nyota wawili wa Barca, Andres Iniesta naLuis Suarez - ambao wote wamepewa alama 89 wanakalia nafasi ya sita na saba, wakati nyota wawili wa Bayern Munich, Bastian Schweinsteiger na Franck Ribery (wote pointi 88) wanashika nafasi ya nane na tisa.
Winga wa Chelsea, Eden Hazard, waliyepata pointi 88 mwaka jana, ni mchezaji pekee wa ligi kuu England aliyeingia 10 bora, akiwazidi kete nyota wa Manchester United Robin van Persie na Radamel Falcao.
0 comments:
Post a Comment