
MANCHESTER United ilikamilisha usajili mkubwa
katika dakika za mwisho za dirisha la usajili la majira ya kiangazi mwaka huu kwa
kuinasa saini ya mshambuliaji hatari, raia wa Colombia, Radamel Falcao.
Falcao
amelijenga jina lake na kuwa moja ya washambuliaji wazuri na hatari zaidi
barani ulaya kwa miaka mitano iliyopita na mpaka hivi sasa.
Huyu
ni mshambuliaji aliyefunga mabao 41 katika mechi 52 za ligi alizoichezea FC
Porto na alifunga mabao 52 katika mechi 68 alizokipiga Atletico Madrid.
Akiwa
AS Monaco ya Ufaransa katika msimu wake wa kwanza alishindwa kuonesha makali
yake kutokana na majeruhi, lakini bado alifunga mabao 11 katika mechi 20
alizocheza.
Hakuna
mtu mwenye wasiwasi juu ya ubora wake licha ya kusumbuliwa na majeruhi. Ni mshambuliaji
hatari na anajua kuzitafuta nyavu.
LAKINI
MANCHESTER UNITED WALIMHITAJI FALCAO WAKATI WANA ROBIN VAN PERISIE NA WAYNE
ROONEY?
Ndiyo.
Ni mchezaji mzuri. Kiwango cha Robin van Persie hakijawa kizuri tangu alipoanza
kucheza msimu wake wa kwanza akiwa United. Wayne Rooney hajawa na muendelezo
mzuri wa kufunga mabao. Amefunga mabao 20 tu kwa misimu miwili tangu
alipojiunga na Man United mwaka 2004. Misimu mingine amekuwa akipanda na
kushuka. Sio mashine ya magoli kama alivyo Falcao.
Falcao
ana uwiano mzuri wa mabao kwa kila dakika kuliko Rooney na van Persie. Ni
mshambuliaji wa aina yake. United imefunga mabao mawili katika mechi zake tatu
za mwanzo wa msimu huu na kwa mazingira hayo wanahitaji mfungaji mzuri zaidi.
Falcao amesajiliwa kwa ajili ya kumaliza ukame huo.
Matokeo
ya usajili huu inawezekana ukamfanya Falcao aanze na Rooney na kumuacha benchi
RvP.
Kama
sio hivyo tunaweza kumuona Wayne Rooney akicheza namba 10 katika mfumo wa
3-4-1-2, nyuma ya Falcao na RvP ambapo itakuwa safu kali ya ushambuliaji.
Au
uwezekano wa mwisho ni kwamba Rooney anaweza kurudishwa nyuma kama kiungo wa
kati sambamba na Darren Fletcher.
Hii
itamruhusu Juan Mata kucheza nyuma ya washambuliaji. Mfumo huu utakuwa wa
hatari zaidi, lakini uwiano wa kikosi utakosekana. United hawaja huru kufunga
mabao mengi kwasababu mfumo ndio umekuwa tatizo.
Walicheza
mipira mirefu dhidi ya Burnley na kiujumla walikosa mawazo sahihi ya kufunga.
Wakiwa na Falcao watakuwa na kitu cha ziada, lakini sio tiba ya matatizo yao
mengine.
Wanahitaji
kutengeneza nafasi nyingi na kuwa na ushirikiano mzuri katika timu. Uhusiano
kutoka safu ya ulinzi na ushambuliaji unahitaji kuboreshwa. Falcao hataweza kufunga
peke yake, hata kama atapata nafasi nyingi.
Kiukweli
ni usajili mzuri, lakini United inahitaji kufanya vitu vingi na kuboresha
maeneo mengine ya timu.
0 comments:
Post a Comment