
ARSENAL ilihitaji mshambuliaji, hakuna wasiwasi
juu ya hilo. Walimsajili Danny Welbeck dakika za mwisho za dirisha la usajili
la majira ya kiangazi mwaka huu na kukifanya kikosi chao kuwa imara zaidi ya
msimu uliopita.
Washika bunduki hao wa London walimuuza Thomas
Vermaelen kwenda klabu ya FC Barcelona na kwa bahati mbaya hawajasajili mrithi
wake.
Walimsajili beki wa kulia kutoka Southampton,
Calum Chambers, lakini wamemtumia kama beki wa kati kwasababu ya majeruhi. Sio mbaya
kumchezesha beki ya kati, lakini kupambana na baadhi ya washambuliaji wa kati wa
kiwango cha juu waliopo timu pinzani inaweza kuzua tatizo.
Hapa hawajaziba pengo. Kwanini Arsene Wenger
hakusajili beki wa kati?. Ilionekana wazi kuwa muhimu kumsajili beki wa kati
mwenye uzoefu, lakini haijafanyika.
Arsenal wamekuwa katika wasiwasi kutokana na
kukosa mabeki wengi wa kati. Mbaya zaidi, kwa majira yote ya kiangazi wamemfukuzia
Morgan Schneiderlin bila mafanikio na kiukweli walihitaji beki asilia wa kati.
Aaron Ramsey ni mzuri kwenye boksi. Jack Wilshere
anashambuliaji zaidi na Mikel Arteta sasa ana miaka 32, hivyo kasi yake imeshuka.
Arteta ni mchezeshaji mzuri, lakini amekosa kasi
ya kupambana na wapinzani na kushindwa kushinda mipira kirahisi. Katika mechi
dhidi ya timu kubwa msimu uliopita, Arsenal alipata shida kutokana na hili.
Kwa mfano katika mechi dhidi ya Chelsea na
Liverpool, Arsenal walifungwa mabao 6-0 na 5-1. Arteta alihangaishwa mno katika
mechi hizi mbili.
Kusajili beki asilia wa kati mwenye nidhamu na
mbinu za kimpira kungekuwa na maana kubwa kwa Arsenal.
Hili lilikuwa janga tena. Kikosi cha Arsenal
kimeimarishwa kwa kuwasajili Alexis Sanchez na Welbeck kuongeza ubora wa safu
ya ushambuliaji na kuwa na machaguo mengi sehemu ya mbele, lakini katika mechi
kubwa msimu uliopita waliruhusu magoli mengi, lakini hawajaboresha eneo la safu
ya ulinzi mpaka sasa.
Safu yao ya ulinzi itayumbishwa na timu bora
pinzani zenye washambuliaji wakali. Safu ya kiungo ilihitaji kuboreshwa, hali
kadhalika safu ya ulinzi ilihitaji mabeki wa kiwango cha juu.
Kama Arsenal watapambana tena kuisaka nafasi ya
nne msimu huu, lawama zote itabidi aangushie kocha mkuu Arsene Wenger
aliyeshindwa kusajili mpaka siku ya mwisho.
0 comments:
Post a Comment