
CHELSEA
walikuwa kimya siku ya mwisho ya usajili. Hakukuwa na ‘presha’ Stamford Bridge
tofauti na kwa wapinzani wao wa Old Trafford, Emirates na kwingineko.
Chelsea
walimaliza biashara yao mapema na walitumia siku ya mwisho ya usajili kuwatoa
kwa mkopo nyota wake makinda. Kulikuwa na utulivu mno. Hali kama hii inaweza
kuzungumzwa kwa Manchester City walioachia wachezaji wao wachache siku ya
mwisho.
Chelsea
walihitimisha biashara yao kwa idadi sahihi ya wachezaji wa kigeni katika
kikosi chao (baada ya kumuachia Marco van Ginkel kujiunga na AC Milan kwa
mkopo) na kumbakisha golikipa wao kwa miaka 10, Petr Cech.
Kumbakisha
Cech lilikuwa jambo zuri mno katika siku ya mwisho ya usajili. Cech alihusishwa
kujiunga na PSG na Monaco baada ya kuanza kusugua benchi.
Uzoefu
wake ni muhimu wakati huu Courtois ameanza msimu wake wa kwanza. Na kama kipa
huyo atachemsha, basi Jose Mourinho atamrejea Cech. Hili linawezekana kwasababu
kuna suala ka majeruhi pia.
Chelsea
kwa sasa ina walinda mlango wawili wa kiwango cha dunia, Arsenal haina hata
mmoja.
Chelsea
walitatua udhaifu wao mkubwa. Diego Costa alianza vizuri kwa kufumania nyavu
mara nne katika mechi tatu. Cesc Fabregas ameongeza nguvu na ubunifu sehemu ya
kiungo. Courtois amekuwa kipa wa kwanza, Filipe Luiz amerithi mikoba ya Ashley
Cole. Unaonekana kuwa usajili mzuri.
Uwepo
wa Louc Remy aliyefunga mabao 20 katia mechi 40 za ligi ni jambo zuri na
limeboresha zaidi kikosi kuliko wakati ule wa Demba Ba au Fernando Torres. Safu
ya ushambuliaji ya Chelsea inaonekana kuwa nzuri zaidi.

0 comments:
Post a Comment