
MANCHESTER United wamekuwa wakitumia
fedha kama ‘vichaa’ tangu msimu uliopita. Pia wamekuwa sugu katika matumizi ya
hali ya juu kwa wakati wote.
Tangu msimu uliopita wametumia fedha
zinazokadiriwa kufikia paundi milioni 218. Ni kiwango kikubwa mno cha fedha.
Hawajaacha tabia hii na matumizi yao
halisi mpaka sasa ni paundi milioni 185. Hiki ni kiwango cha juu kuliko klabu
yoyote ya ligi kuu ndani ya muda kama huo. Kiukweli dirisha la usajili kwa
United limevunja rekodi.
Mitandao ya kijamii imechanganyikiwa
na inaikosoa United kwa matumizi makubwa. Wengine wameenda mbali kwa
kuifananisha United na Manchester City au Chelsea. Matumizi ni makubwa, lakini
kuifananisha na klabu hizo sio haki.
Manchester United wanaweza kutumia zaidi
kwasababu wamejijenge vizuri katika
mfumo wao wa soka la vijana (The Class of 92). Wakati huo United ikiwa chini ya
Sir Alex Ferguson ilijijenga kuwa klabu yenye nguvu zaidi kifedha duniani.
Hizi ndizo fedha wanazoweza kutumia.
United imeingia mikataba mikubwa na Adidas, Chevrolet na kadhalika. Na hii ndio
inawafanya wawe na uwezo mkubwa wa fedha na mapato yao yanawafanya watumie
fedha nyingi.
Wakati ambao Chelsea na City walitumia
fedha nyingi hawakuwa na mapato makubwa na matumizi yale yaliwapatia kadi
nyekundu. Kutoka hapo Cheslea na City wamekuwa na tahadhari kubwa katika
matumizi ya fedha.
United wanaweza kutumia fedha nyingi kwasababu mapato yao ni makunwa, kwa
muda mrefu wamekuwa katika klabu nne za juu na wamekuwa na mapato makubwa. Mafanikio
haya yamewafanya watumie fedha nyingi.
Matumizi yao ni tofauti kabisa na ya
Chelsea na City. Umwamba wao katika mapato unawafanya wawe na uwezo mkubwa wa
kifedha.
Ni matumizi mabaya?. Si sababu ya
kimpira zaidi, lakini sio matumizi mabaya. United wamejijenga kwa muda mrefu.
Chelsea imekuwa timu kubwa ndani ya miaka 10 iliyopita, shukurani kwa Roman
Abramovich.
Kama United hawataingia timu nne za
juu msimu huu litakuwa tatizo kwao. Kwa sasa matumizi yao yanafahamika,
yawezekana ni mazuri ingawa ni makubwa sana.
0 comments:
Post a Comment