Mshambulaji wa Coastal Union
aliysajiliwa kutoka timu ya Gormahia ya
Kenya
Itubu Imbem kushoto akiwa na Meneja wa timu ya Coastal
Union,Akida
Machai mara baada ya kusaini mkataba wa miaka mwii wa
kuitumia
timu hiyo hivi karibuni
Na Mwandishi Wetu, Tanga
MSHAMBULAJI
wa Klabu ya Coastal Union Itubu Imben raia wa Kongo aliyetokea timu ya Gorhamia ya Kenya Itubu Imbem jana
alianza kuonyesha
cheche zake baada ya kuifungia timu hiyo mabao matatu wakati Coastal Union ikiifunga Falcon FC ya Pemba mabao
10-0,katika mchezo wa kirafiki
uliofanyika kwenye uwanja wa soka Gombani.
Falcon
Fc inashiriki Michuano ya Ligi daraja la kwanza visiwani humo ambapo
ilikutana na dhahama hiyo ya mabao kutoka kwa wachezaji mahiri ambao wamesajiliwa msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom
Tanzania bara.
Wakionekana
kujiamini na kujipanga vilivyo,Coastal Union waliweza kuendeleza
wimbi la mashambulizi langoni mwa wapinzani wao hao na kufanikiwa
kupata mabao hayo ambapo mpaka timu hizo zinakwenda mapumziko
Coastal Union walikuwa mbele kwa mabao 5-0.
Mabao
ya Coastal Union mengine yalifungwa na Abasi Athumani ambaye alipachika
mabao matatu kwenye mchezo huo wakati Mahundi Petro na Mbwana
Hamisi kila mmoja akipachika bao moja langoni mwa timu hiyo.
Katika
kuhakikisha Coastal Union inaendelea kuibuka na idadi kubwa ya mabao
iliweza kuendelea kasi ya mashambulizi langoni mwa Falcon na kufanikiwa
kuandika mabao mengine ambapo Rama Salim mchezaji mahiri naye
aliyetokea klabu ya Gormahia ya Kenya ambaye pia aliwahi kuichezea
Harambee Stars ya nchi hiyo aliweza kuandika mabao mawili na kuhitimisha
karamu ya mabao.
Akizungumzia
hali ya kikosi hicho,Kocha Mkuu wa timu hiyo,Yusuph Chippo
alisema kuwa kutokana na maandalizi waliyoyafanya wakiwa visiwani
humo wanamatumaini makubwa ya kufanya vizuri katika michuano ya
Ligi kuu soka Tanzania bara itakayoanza Septemba 20 mwaka huu.
“Ninaweza kusema hivi kuwa sasa kikosi changu kimeimarika kwani hapo
juzi tuliifunga timu ya Opec ya Visiwani hapa mabao 11-0 hivyo kikosi
changu kipo tayari kushiriki michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara
msimu ujao na hasa tukianzia na mechi yetu na Simba kwa kuchukua pointi
tatu muhimu “Alisema Chippo.


0 comments:
Post a Comment