Kitu cha pili: Danny Welbeck akiifungia England bao la pili.
ROY HODGSON ameiongoza England kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Uswizi katika mechi ya kwanza ya kuwania kufuzu fainali za Euro 2016.
Ikitumia mfumo wa 4-4-2, England ilijitahidi kuonesha soka safi na kushinda mechi ambayo pengine ilikuwa ngumu zaidi kwake katika kampeni za kufuzu fainai za mataifa ya Ulaya.
Mshambuliaji mpya wa Arsenal aliyesajiliwa kutoka Manachester United, Danny Welbeck alifunga yote mabao mawili katika mechi hiyo.
Welbeck alifunga bao la kwanza dakika ya 59 na bao la pili alifunga dakika ya 90 na kuizamisha Uswizi inayochipukia kwa kasi katika soka la Ulaya.
Alipiga vidude viwili: Welbeck akifunga bao mjini Basle
Mtu muhimu: Welbeck, akitokea kusajili kwa paundi milioni 16 na kujiunga na Arsenal alifanya kazi nzuri.
Kikosi cha Switzerland (4-3-2-1): Sommer 5.5, Lichsteiner 6.5, Djourou 6, von Bergen 5.5, Rodriguez 6, Behrami, 6.5, Inler 7, Mehmedi 6 (Drmic, 63), Xhaka 7 (Dzemaili 74, 5.5), Shaqiri 8, Seferovic 7
Wachezaji wa akiba ambao hawkautumika: Hitz, Benito, Senderos, Widmer, Frei, Stocker, Fernandes, Kasami, Schar, Burki.
Kikosi cha England (4-4-2): Hart 7, Stones 6, Cahill 7, Jones 6 (Jagielka 77), Baines 6.5, Wilshere 6 (Milner 73, 6), Henderson 6, Delph 6.5, Sterling 6.5, Welbeck 8, Rooney 6.5 (Lambert 90).
Wachezaji wa akiba ambao hawakucheza: Forster, Rose, Chambers, Oxlade-Chamberlain, Townsend.
Mfungaji wa magoli: Welbeck 59, 90
Kadi ya njano: Delph, Lambert
Mwamuzi: Cuneyt Cakir 6
Watazamaji: 35,500

0 comments:
Post a Comment