
Na Mwandishi Wetu, Tanga
TIMU ya Coastal Union ya Tanga jana iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Morogoro ikiwa ni kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani ikiwa ni siku maalumu ya Coastal Union Day ambayo huazimishwa kila mwaka kabla ya kuanza msimu mpya
Baada ya kumalizika mchezo huo kulifanyika utambulisho kwa wachezaji waliosajiliwa kwa wapenzi,mashabiki na wanachama waliojitokeza kushuhudia mchezo huo.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa vuta ni kuvute kutokana na timu zote kuonyesha kandanda safi na la kuivutia ambapo mpaka timu zote zinakwenda mapumziko, Coastal Union iliweza kutoka kifua mbele kwa kufunga bao 1-0 ambalo lilifungwa na Ramadhani Salim baada ya kuunganisha mpira wa kona uliopigwa na Bakari Mtama.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo timu zote ziliingia uwanjani hapo zikiwa na nguvu mpya baada ya kufanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji wao ambapo Coastal Union iliwatoa Amani Juma, Abdallah Mfuko, Imbem Itubu ambao nafasi zao zikichukuliwa na Hamadi Hamis,Ike
Bright Obina .
Ambapo kwa upande wa Polisi Morogoro wao waliwatoa Gilbert Salehe,Fedilis Sanja,Hussein mwamwanda na kuwaingiza Elias Mashaka ,Nelson Kassian na Msafiri Chelula ambapo waliibadilisha timu kipindi
hicho kwa kupeleka mashambulizi mara kwa mara langoni mwa Coastal
Union bila mafanikio yoyote.
Kutokana na shambulizi hilo, Coastal Union nao waliweza kujipanga na kufanya shambulizi la nguvu langoni mwa Polisi Morogoro na hatimaye kuweza kuandika bao la pili lililowekwa kimiani na Ike Bright Obina baada ya kumalizia mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Bakari Mtama.
Akizungumza mara baada ya kumalizika mchezo huo,Kocha Mkuu wa Coastal Union,Yusuph Chippo alisema kuwa timu hiyo kuendelea kupata matokea mazuri kwenye mechi zao za majaribio ni salamu tosha kuwa itakuwa
tishio katika msimu mpya wa Ligi kuu soka Tanzania bara.

0 comments:
Post a Comment