
NASSIB Abdul ‘Diamond Platnumz’ ni msanii wa
muziki wa kizazi kipya ‘Bongo Fleiva’ anayetikisa ndani na nje ya nchi kwa
sasa.
Mkali huyu wa kibao cha ‘Number One na Mdogo mdogo’
amejizolea umaarufu mkubwa na kuteka soka la mashabiki nchini Tanzania, nchi za
Afrika mashariki na kati, sehemu kadhaa za Afrika magharibi na kwingineko, bila
kusahau duniani kote.
Kutokana na ufanisi wa kazi zake, Diamond amekuwa
msanii wa kipekee na anakusanya mkwanja mrefu pengine kuliko wasanii wote, kwa
rekodi za miaka ya karibuni.
Lakini wengi wakisikia jina la Diamond, basi
wanarejea vibayo vyake vingine vya sasa na zamani. Nyimbo kama Nenda kamwambie,
Mbagala, Nalia na Mengi, Mawazo, Nimpende Nani, Ukimwona, Nataka kulewa, My
Number One na sasa Mdogo Mdogo, hakika zinapigwa na kusikilizwa sana.
Pia amekuwa na shoo za bei mbaya ndani na nje ya
nchi. Hutumika katika matangazo ya makampuni makubwa na kuingiza pesa ndefu.
Yapo mengi ya kumzungumzia Diamond katika maisha
yake ya muziki, lakini leo tunaangazia maisha ya upande wa pili, hususani
michezo.

Daimond anamkubali sana bondi Floyd Mayweather
Nyota huyu wa muziki alikiri kuwa zamani alikuwa
anapenda sana michezo hususani mchezo wa ngumi, lakini akaachana nao na kuingia katika soka.
Alisema: “Zamani nilikuwa napenda sana michezo,nilikuwa
napenda ngumi ‘Boxing’, lakini nikaona
mambo ya kupigana hapana!”
“Pia nikaanza kucheza mpira. Nilicheza vizuri tu, lakini
kuna vitu vilinikatiza hasa mama yangu ambaye hakupenda nicheze mpira.
kwasababu kuna jirani yetu alipata matatizo, waligongana miguu na akavunjika.”
“Kila nikitaka kuendelea kucheza, basi mama
anasema unafahmu fulani alivunjika kwasababu ya mpira, kila nikifiria daaah! Nilikuwa
naogopa na kuona kweli naweza kuvunjika miguu. Kuanzia hapo nikaacha kabisa
mpira mpaka leo na nikawa napenda muziki”
Kama ilivyo kawaida kwa vijana wengi, huwa wanapenda
kuzishabikia klabu kongwe mbili nchini, Simba na Yanga, kwa upande wa Diamond
hali ikoje?
“Nilipokuwa mdogo nilikuwa nafuatilia Simba,
lakini ilikuwa mkumbo.

Mrisho Ngassa
Nikisikia wengine wako Yanga basi namimi Simba, lakini
nilikuwa sielewi.”
“Kiukweli sijui ni timu ipi kwasababu sijakaa sana
kafuatilia. Nisikia watu wengi wapo Yanga, kwahiyo naona nikisema Yanga
nitakuwa kama nimefuata mkumbo”. Alisema Diamond.
Kichekesho cha aina yake ni kwamba, katika
wachezaji wote wanaocheza soka la Tanzania kwa sasa, Diamond anamjua mchezaji
mmoja tu ambaye ni mshambuliaji wa Yanga
na Taifa Stars, Mrisho Khalfan Ngassa.
“Ngassa mwanangu. Nilikuwa nasikia anatajwa sana,
nikaja kukutana naye na tukafanya Tangazo. Nikaona ni mtu poa na kuanzia hapo
akawa mwanangu. Muda mwingi akawa ananipigia akisema mwanangu sisi tunaenda
kucheza mpira sehemu fulani”
“Kwahiyo ukisema niangalie mpira, nitasema Ngassa
tu kwasababu ndio ninayemfahamu na ni mwanangu”.
Kama kawaida, wasanii wengi kama akina Madee,
Chege, Professor Jay na wengine wanafuatilia sana klabu za nje kama Manchester
United, Liverpool na nyinginezo, lakini kwa Diamond je?
“Kuna kipindi nilikuwa nakaa Kariakoo na nilikuwa
naipenda sana Barcelona kwasababu alikuwepo huko Eto’o. Mpaka sahizi najua
Messi yupo, na siku za karibuni, Neymar. Zamani nilikuwa naweza kutaja namba
zote, lakini sahizi sikumbuki” alisema mwanamuziki huyo maarufu.
Kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram,
Diamond amewafuata baadhi ya wachezaji nyota kama Samuel Eto’o, Didier Drogba,
Emmanuel Adebayor, na bondi Mayweather, kwanini hao na sio watu wengine?
“Nimekuwa nikiwasikia sana. Wanacheza halafu ni ‘mastaa’.
Kila nikipita mitaani nawasikia, basi nikaona ngoja niwafuate” Alisema Diamond.
“Kuhusu Myweather, yaani ni mtu staa sana, mtu wa mashauzi
kinoma, matanuzi, ananifurahisha sana. Mara aposti mademu zake, mara magari
yake, fedha zake…nampenda sana”.
Wapenzi wengi wa soka ukiwapa nafasi ya kuchagua
ni mchezaji gani wana ndoto ya kuonana naye ana kwa ana, kila mtu atataja wake
kutokana na mapenzi makubwa aliyonayo, kuhusu Diamond hali ikoje?
“Nina ndoto ya kukutana na Messi kwasababu namjua
toka anaanza Barcelona, alivyoanza kuchez mpaka anakuwa staa. Ni mtu wa kazi.
Kwa juzi juzi alipokosa tuzo ya mchezaji bora wa dunia, iliniuma sana”.

0 comments:
Post a Comment