
Na
Baraka Mpenja, Dar es salaam
MBRAZIL
Marcio Maximo leo majira ya saa 11:00
jioni anatarajia kuiongoza Yanga katika mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya
Thika United ya Kenya ndani ya dimba la Taifa jijini Dar es salaam.
Mechi
hii ni muendelezo wa mechi za kujipima ubavu kabla ya kuanza kwa ligi kuu soka
Tanzania bara inayotarajia kuanza kushika kasi septembe 20 mwaka huu ambapo
Yanga wataanza kampeni zao za kusaka ubingwa dhidi ya Mtibwa Sugar katika dimba
la Jamhuri mkoani Morogoro.
Mchezo
na Thika United ni kipimo kizuri kwa Maximo ambaye alifanya vizuri katika mechi
za kirafiki alizocheza Zanzibar ambapo wachezaji wote walionesha viwango vya
hali ya juu.
Viingilio
katika mechi ya leo ni shilingi elfu 30,000 kwa VIP A na shilingi 20,000 kwa
VIA B.
Viti
vya rangi ya chungwa ni shilingi 10,000, wakati viti vya rangi ya kijani na
bluu kiingilio ni buku tano tu (5,000/=).

Hata
hivyo, kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mbrazil, Andrey Coutinho anatarajia kuwa
kivutio katika mchezo wa leo kutokana na
kiwango kikubwa alichoonesha katika mechi za kirafiki visiwani Zanzibar.
Coutinho
alifunga mabao 2 katika mechi 3 alizocheza Zanzibar. Alifunga bao moja moja
katika mechi mbili dhidi ya Shangani na KMKM, Yanga ikishinda mabao 2-0 kwa
mechi zote.
Mbali
na kufunga mabao hayo alionekana kuwa na kasi nzuri uwanjani, alimiliki vizuri
mipira na kupiga pasi kwa ufundi mkubwa.
Pia
alionekana kuwa na uwezo mzuri wa kupiga kona na mashuti ya mbali.
Kwa
mashabiki wa Yanga waliopo jijini Dar es salaam watapata fursa nzuri ya kumuona
Coutinho akifanya vitu vyake katika dimba la Taifa.
Kwa
Mbrazil mwingine, Geilson Santos Santana ‘Jaja’ hakuonesha kiwango kikubwa
katika mechi za Zanzibar licha ya kufunga bao pakee katika ushindi wa 1-0
iliopata Yanga dhidi ya Chipukizi FC uwanja wa Gombani Pemba.
Jaja
anatakiwa kuonesha kiwango leo hii ili kuwapa imani mashabiki wa Yanga.
Mbali
na Wabrazil hao wawili, wachezaji wengine watakuwa na kibarua cha kuonesha
makali yao mbele ya Marcio Maximo mwenye rekodi ya kushinda mechi zote tatu za
kirafiki alizocheza mpaka sasa.
0 comments:
Post a Comment