
Kazi ngumu: Neville alitambulishwa rasmi kufanya kazi ya uchambuzi kwenye TV wakati wa kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu nchini Brazil.
Imechapishwa Agosti 7, 2014, saa 6:30 mchana
PHILI Neville amepiga chini kazi ya ukocha chini ya Louis Van Gaal katika klabu ya Manchester United na msimu ujao atakaa kwenye sofa za TV kuchambua mechi.
Baada ya kutangazwa kuwa miongoni mwa watu wanaounda timu ya MOTD katika harakati zake za kutimiza miaka 50 ya kutangaza ligi, Neville aliwaambia wafuasi wake milioni moja kwenye mtandao wa Twita kuwa hataendelea tena na kazi ya ukocha Manchester United ambapo alifanya kazi kama kocha msaidizi wa kikosi cha kwanza chini ya David Moyes msimu uliopita.
Aliulizwa: 'Phil bado unaendela kuwa kocha United? alijibu: 'Hapana'.

Beki huyo wa zamani ametangaza kuwa hataendelea kuwepo Manchester United kama kocha msaidizi.
Baadaye, United ilisema kuondoka kwa Neville ni maamuzi yake na klabu ilipenda sana kuendelea naye sambamba na wenzake wa kikosi cha 'Class of 92', Ryan Giggs na Bicky Butt.
Lakini watajaribu kuzungumza na Neville ili kuona kama anaweza kubakia Manchester United kwa namna nyingine, inawezekana kuwa Balozi wa timu katika masuala ya kijamii.
Msemaji wa United alisema: 'Bado tunasema kuwa tulimhitaji na hatukujua kama kazi yake ya Tv ingemtoa kama ilivyotokea kwa kaka yake Gary.'
Neville mwenye miaka 37 aliyekosolewa vikali baada ya kuisema vibaya England kwenye mechi dhidi ya Italia katika fainali za kombe la dunia nchini Brazil, ameamua kujikita zaidi na kazi yake ya utangazaji.

Uthibitisho: Neville aliandika kwenye Twita kuthibitisha kuwa hatakuwepo tena Manchester United katika nafasi ya kocha msaidizi.
0 comments:
Post a Comment