
Na Baraka Mpenja
MABINGWA wa Tanzania bara, Azam fc watachuana na
El Merreikh ya Sudan katika mchezo wa robo fainali ya klabu bingwa Afrika
mashariki na kati, kombe la Kagame siku ya jumatano kwenye uwanja wa Nyamirambo,
mjini Kigali, nchini Rwanda.
Hii inatokana na wenyeji Rayon Sports kumaliza
kundi A wakishika nafasi ya kwanza kwa kujikusanyia pointi 10 kufuatia ushindi
wa 1-0 dhidi ya Altabara ya Sudan kusini.
Bao pekee la ushindi la Rayon limefungwa katika dakika
ya 87 kupitia kwa Motombo Govin.
Kwa matokeo ya leo, kundi A linaongozwa na Rayon
wenye pointi 10, wakifuatiwa na Azam fc waliojikusanyia pointi 8 katika nafasi
ya pili, huku Altabara wakishika nafasi ya tatu kwa pointi 3 na wanakwenda Robo
fainali pia.
Rayon inaweza kukabiliana na KCC ya Uganda au APR
ya Rwanda kutegemeana na matokeo ya mechi za mwisho katika kundi B hapo kesho.
Mapema katika uwanja huo wa Nyamirambo, Azam fc
walijizolea pointi tatu muhimu dhidi ya Adamma City ya Ethiopia baada ya
kuitungua mabao 4-1.
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika kwa
sare ya bao 1-1 ambapo Azam walikuwa wa kwanza kufunga kupitia kwa Bocco
akiunganisha krosi ya Khamis Mcha ‘Vialli’, lakini Desaleny Bebesh
aliisawazishia Adamma katika dakika ya 39.
Katika dakika 55, Kavumbagu alifunga bao la pili
akimalizia krosi ya Erasto Nyoni.
Dakika ya 60 Mcha alifunga bao la tatu baada ya
kuuwahi mpira uliotemwa na mlinda mlango wa Adamma na katika dakika ya 74
Tchetche alihitimisha karamu ya mabao.

0 comments:
Post a Comment