Safari ya Jose Mourinho ya kutafuta ubingwa inaanza jumatatu
Katika
mechi nyingine, Leicester City watacheza mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu
England tangu mwaka 2004 watakapoikaribisha Everton leo, wakati timu nyingine
iliyopanda msimu huu, Queens Park Rangers itachuana na Hull City Uwanja wa
Loftus Road. Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu,
Manchester City wataanza kutetea taji lao dhidi ya Newcastle United kesho. Liverpool, wataanza kampeni zao
dhidi ya Southampton, ambao wamewauza Adam Lallana, Rickie Lambert na Dejan
Lovren kwa Wekundu hao wa Anfield. Chelsea ya Mreno Jose Mourinho,
ikiongozwa na wachezaji wake wapya, Diego Costa na Cesc Fabregas itakabiliana
na Burnley iliyopanda msimu huu Jumatatu. Mechi nyingine; Stoke City na Aston
Villa, West Bromwich Albion na Sunderland na West Ham United dhidi ya Tottenham
Hotspur, wakati kesho Liverpool v Southampton, Newcastle United v Manchester
City na keshokutwa Burnley v Chelsea.
|
0 comments:
Post a Comment