Thursday, August 21, 2014

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

MTIHANI wa kwanza wa kocha wa Yanga sc, Brazil, Marcio Maximo ni leo hii ambapo atawaongoza vijana wa Jangwani kuoneshana ujuzi na timu ya Chipukizi FC ya Zanzibar.

Maximo ambaye amekinoa kikosi chake kwa zaidi ya mwezi mmoja tangu arithi mikoba ya Mholanzi, Hans Van der Pluijm, anatarajia kuwatumia wachezaji wote wa kikosi cha kwanza na cha pili ili kuona namna walivyopokea mafunzo yake yaliyofanyika kwa muda mrefu uwanja wa shule ya Sekondari, Loyola, iliyopo Mabibo jijini Dar es salaam.

Ingawa mechi hii itakayoanza majira ya saa 10:00 jioni uwanja wa Gombani, Kisiwani Pemba ni ya kirafiki, lakini ina umuhimu mkubwa kwa Maximo kwasababu anahitaji kuwaaminisha mashabiki wa Yanga wenye imani kubwa na mwalimu huyu wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ (2006-2010).

Viingilio katika mechi hiyo ni shilingi elfu tatu (3,000/=)  kwa VIP na elfu mbili (2,000/=)  majukwaa ya kawaida.

Mashabiki wa Yanga waliopo Pemba na Zanzibar wanatarajiwa kufurika Gombani kuwaona vijana wa Yanga, hususani Wabrazil wawili, Gleilson Santos Santana ‘Jaja’ na Andrey Coutinho ambao kwa mara ya kwanza watacheza mechi ya kirafiki tangu wasajiliwe majira haya ya kiangazi.

Kocha mkuuu Marcio Maximo na kikosi chake wamefikia katika hoteli ya kitalii ya Pemba Misali iliyopo eneo la Wesha na watajifua kwa takribani siku 10 kabla ya kurejea jijini Dar es salaam mwishoni mwa mwezi huu.

Kulingana na program ya bench la Ufundi kisiwani Pemba, Young Africans inatarajia kucheza michezo mitatu ya kirafiki na timu za kutoka Visiwa vya Pemba na Unguja na baadaye kurejea Dar es salaam kwa michezo miwili ya kimataifa kabla ya kucheza mchezo wa Ngao ya Hisani septemba 13, 2014.

Wachezaji waliopo Pemba Walinda Mlango Juma Kaseja, Ally Mustafa "Barthez" na Deogratias Munish "Dida", Walinzi wa Pembeni, Juma Abdul, Salum Telea, Oscar Joshua, Edwad Charles na Amos Abel

Walinzi wa Kati ni Kelvin Yondani, Nadir Haroub "Cannavaro", Rajab Zahir na Pato Ngonyani.

Viungo: Mbuyu Twite, Said Juma "Makapu", Omega Seme, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima na Hamis Thabit.

Viungo wa Pembeni: Saimon Msuva, Mrisho Ngasa, Nizar Khalfani na Andrey Coutinho.

Washambuliaji: Geilson Santos "Jaja", Said Bahanuzi, Jerson Tegete, Hamis Kizza na Hussein Javu 

Benchi la Ufundi walioko Kisiwani Pemba ni:

Kocha Mkuu : Marcio Maximo

Kocha wasaidizi Leonado Neiva, Salvatory Edward

Kocha wa Makipa:  Juma Pondamali

Daktari wa timu: Dr Suphian Juma

Meneja wa timu:  Hafidh Saleh

Mchua Misuli: Jaco Onyango


Mtunza Vifaa: Mahmod Omar "Mpogolo" 

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video