
Imechapishwa Agosti 3, 2014, 2014, saa 11:27 jioni
KLABU ya Simba imefanya mkutano mkuu wa wanachama
leo hii katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Osterbay jijini Dar es
salaam kujadili masuala mbalimbali ya klabu hiyo.
Mkutano huo ni wa kwanza tangu viongozi wapya
chini ya Rais Evans Eliaza Aveva na makamu wake Geofrey Nyange ‘Kaburu’ waingie
madarakani juni 29 mwaka huu.
Agenda za mkutano huo zilitangazwa jana na Agenda
ya 11 ambayo ilihusu wanachama 72 waliosimamishwa uanachama na kamati tendaji
ilitegemewa kuwa ya vuta ni kuvute.
Kama ilivyotabiriwa jana, leo hii agenda hiyo
ilivuta hisia za wengi na mwisho wa siku taarifa kutoka kwenye mkutano huo zinaeleza
kuwa mkutano mkuu umeamua kuwafuta uanachamama (kuwafukuzwa) wale wote
walioipeleka Simba mahakamani.
Idadi ya wanachama 72 pamoja na aliyekuwa mgombea
wa Urais wa klabu hiyo, Michael Richard Wambura wamefutwa na kufukuzwa kabisa.
Taarifa zinaarifu kuwa maamuzi hayo yamechukuliwa
na wanachama zaidi ya 600 waliohudhuria mkutano huo.
Wambura aliipeleka Simba mahakamani mwaka 2010
wakati wanachama wengine waliobaki waliipekea klabu mahakama kuu kanda ya Dar
es salaam wakitaka uchaguzi mkuu
uliofanyika juni 29 mwaka huu usimamishwe kwa madai kuwa katiba ilikiukwa na
kamati ya uchaguzi ya Simba chini ya mwenyekiti wake, mwanasheria, Dkt. Damas
Wambura, lakini chanzo kikubwa kilikuwa kuenguliwa kwa Wambura.
Hata hivyo kabla ya ya kufikia maamuzi ya leo,
Rais wa Simba Evans Aveva aliwataka wanachama waliosimamishwa kujitokeza kwake
na kuwasilisha utetezi, lakini hakuna mwanachama aliyefanya hivyo.
0 comments:
Post a Comment