
Imechapishwa Agosti 4, 2014, saa 12:10 jioni
MASHABIKI wa Zamalek walivamia makao
makuu ya klabu hiyo na kuharibu mali za ofisi ya mwenyekiti, Mortada Mansour.
Mansour katika mkutano wake na
waandishi wa habari aliwakosoa na kuwashutumu mashabiki wa klabu hiyo wanaojulikana
kwa jina la ‘White Knights’.
“Kundi kubwa la mashabiki wa ‘White
Knights’ lilivamia makao makuu ya klabu siku ya jumamosi mchana na waliharibu
mali za ofisi ya mwenyekiti, lakini yeye hakuwepo.
“Waliharibu viti, milango na kuwaacha
wafanyakazi wakiwa na hofu kubwa. Mfanyakazi mmoja wa klabu alijeruhiwa,”
Mkurugenzi wa Zamalek, Alaa Mekled aliiambia Supersport.com.
“Tulizungumza na polisi na wataanza
uchunguzi. Pia waliandika maneno mabaya kwenye ukuta yanayomtukana mwenyekiti”
aliongeza.
Mwenyekiti wa klabu Mortada Mansour alisema:
“Niliwaonya wasirudie tena kufanya hivyo, walinzi watawashughulikia. Hawa
watoto sio mashabiki wa kweli wa klabu. Mashabiki wa kweli wanaiunga mkono
klabu kwenye mechi zote ili kutafuta ushindi.
“Nilizungumza na waziri wa mambo ya
ndani, Mohamed Ibrahim na nilimuomba walinzi wawe na bunduki kuilinda klabu.
Kila siku kuna watu zaidi ya 500 wanakuja klabuni na lazima niwalinde.”
0 comments:
Post a Comment